Header Ads Widget

MKUU WA MKOA MTWARA AWAPONGEZA MADAKTARI TOKA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE(JKCI)

 

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanal Ahmed Abbas amewapongeza madaktari bingwa wa moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) 15 waliofika mkoani hapo na kuendesha kambi ya matibabu  ya moyo kwa siku tatu katika hospitali ya kanda ya kusini.


Kauli hiyo ameitoa baada ya kutembelea kambi hiyo na kuona huduma mbalimbali za vipimo na matibabu zikiendelea hospitalini hapo ujenzi na vifaa vimegharimu  bilioni 23.


“ujio wa madaktari bingwa katika hospitali yetu ni faraja sana tunaona watu wengi wana uhitaji mkubwa wa kupata vipimo na matibabu itapendeza kama kila mmoja ataona umuhimu wa kukata bima ya afya ili iweze kuwa mkombozi wa afya yako kwa sababu vipimo na matibabu ya moyo ni gharama kubwa”


“Hospitali ya kanda ya kusini ni moja kati ya hospitali mkombozi katika kanda ya kusini na majirani zetu imepunguza safari za wananchi kwenda mikoa mingine kupata tiba serikali inaendelea kuboresha huduma kwa kuongeza vifaa na mahitaji ya kibingwa muhimu ili kuwezesha madaktari bingwa tulionao kufanya kazi kwa ufanisi zaidi”


Nae Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya alisema kuwa watu wengi wanahitaji huduma za matibabu na vipimo vya magonjwa ya moyo hivyo ujio wa JKCI utasaidia wengi.


“Watu wapo wengi na wamejitokeza imeonyesha wengi wanauhitaji na wameonyesha uzaliendo ni idadi kubwa na uwekezaji ni mkubwa inaonyesha jinsi watu walivyo tayari kupokea huduma hizo” alisema kyobya


Nae Mkurugenzi wa tiba – Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dr Tatizo Waane anasema kuwa mbali na matibabu na vipimo  pia tunafanya utafiti na kwa siku ya kwanza tuliona wagonjwa 160.


“Tumeona wagonjwa watoto na watu wa zima kwa huduma za kibingwa tumekuja na vipimo na tumekuta mashine mbalimbali za moyo zipo hapa tunashukuru kwa kupata nafasi ya kufika hapa na kutoa huduma za vipimo” alisema Waane 


“Zoezi endelevu linafanyika mikoa mbalimbali mwezi uliopita tulikuwa hospitali ya kanda ya chato ambapo tuliona wagonjwa 1000 kati ya hao 200  wanauhitaji wa matibabu zaidi kwenye taasisi yetu” alisema Dr Wanne


nae Kaimu Mkurugenzi wa hospitali ya kanda ya kusini Mtwara Herbet Masigati amesema kuwa serikali imetengeza mazingira wezeshi kwa hospitali ya kanda kutoa huduma za kibingwa.


“Tunaishukuru JKCI kufika hapa wameweza kuendesha zoezi la upimaji na vipimo vya magonjwa ya moyo na muitikio ni mkubwa mwezi wa tisa tulikuwa na madaktari bingwa wa mifupa kutoka MOI walikuja na kutoa huduma hapa tunavyo vifaa vya kutosha kutoa huduma za kibingwa” alisema Masigati.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI