Header Ads Widget

MBUNGE WA JIMBO LA IGALULA AMEDHAMIRIA KUIBUA VIPAJI VYA SOKA VIJIJINI

 

NI Mbunge wa  jimbo la Igalula Venant Protas akiwapati viongozi wa ccm mipira kuashiria uhamasishaji michezo na kuibua vipaji wa kwanza kushoto ni Moshi Mtawo alivaa miwani ni Masudi Kapama na alivevaa kofia nyeupi na wekundu ni Nasibu Mtengwa .

Mbunge wa  jimbo la Igalula Venant Protas akimkabidhi mipira mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha kinamangi kata ya Kigwa   Sadik Mohamed

 James Erick Kabepele aliyesimama katikati akipokea jezi namba 8 kutoka kwa Mbunge wa  jimbo la Igalula Venant Protas  mwengine ni mwanafunzi Wiliud  Patrick

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Uyui Said Ntahondi akipokea jezi kutoka kwa Mbunge wa  jimbo la Igalula Venant Protas na aliyesimama kushoto ni Said Kapoka mdau wa michezo.

Diwani wa kata ya Goweko na makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Uyui kushoto  Shabani Katalambula Akipokea jezi kwa ajili ya timu za Vijiji vya kata hiyo kutoka kwa Mbunge wa  jimbo la Igalula Venant Protas na aliyesimama katikati ni Juma Mrisho.

                            xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Lucas Raphael,Tabora

Mbunge wa jimbo la Igalula wilaya ya uyui mkoani Tabora Venant Protas amekusudia kutekeleza mpango wa kuanzisha ligi ya wilaya hyo  itakayohusisha timu za wilaya nzima ya Uyui hatua ambayo itasaidia kuongeza kasi ya kuibua vipaji kwa vijana hususani waishio vijiji ambao wamekuwa wakisahaulika.

 

Alitoa  kauli hiyo jana alipokuwa akikabidhi vifaa vya michezo katika kata ya kigwa zoezi ambalo amekuwa akilitekeleza katika vijiji  58 vya jimbo la Igalula kama hamasa kwa vijana kupenda michezo.

 

Alisema kuwa wanamichezo wote katika wilaya hiyo kuendelea kujifua kwa ajili mandalizi ya ligi ya wilaya ambayo anakusudia kuanzisha hivi karibuni.

 

Venant alisema michezo ni ajira michezo inadumisha umoja na mshikamano miongoni mwa vijana wa kata moja na kata nyingne .

 

Alisema umoja kwa wanamichezo ni nguzo muhimu kwa vijana ambao wanatarajia kushiriki ligi ya wilaya ya uyui na kuhakikishia vijana hao kuifanya ligi hiyo kuwa bora miongoni mwa ligi katika mkoa wa Tabora  

 

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Uyui, Said Ntahondi alipongeza hatua hiyo ambayo inakwenda kuwa chachu katika kukuza na kuibua vipaji vya soka hapa nchini na kuwataka wadau wengine kuendelea kuwapiga tafu vijana hasa walioko vijijini.

 

Alisema kwamba kuibua kwa vipaji vya wanamichezo vijijini kutasaidia kupatikana kwa wanamichezo waliobora wa miaka ijayo .

 

“Mbunge leo unaona umefanya jambo hili la kutoa vifaa vya michezo kwenye kata 58 lakini jambo ili sio ndogo hata kidogo bali likifanyika kwa kila kata litaibua   vipaji vilivyo bora na  hivyo wilaya ya uyui itatoa samata wa miaka ijayo “alisema Ntahondi

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI