NA TITUS MWOMBEKI, Matukio Daima App Kagera.
MAWAKALA watano kutoka makampuni mbalimbali ya simu za mkononi nchini wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kagera kwa kosa la kuwasajilia watu laini za simu kwa kutumia majina ya watu wengine.
Hayo yamesemwa na mkuu wa TAKUKURU Kagera, John Joseph wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa taasisi hiyo katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu ambapo amesema kuwa makawala hao wanashikiliwa kutokana na kukoswa uadilifu na uaminifu katika utendaji kazi wao.
“Tumeweza kufanya ufuatiliaji pia katika usajili wa laini za simu za mkononi, tumebaini wamekuwepo na baadhi ya mawakala wa makampuni ya simu za mikononi kutoka katika makampuni mbalimbali ambao sio waadilifu wamekuwa wakiwasajilia baadhi ya watu laini kwa kutumia majina ya watu wengine na baadhi ya namba hizo utumika katika uharifu, hivyo tumekamata vijana watano ambao tunaendelea na kufanya uchunguzi wakina na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao pindi uchunguzi utakapokamilika”
“Ni vyema watu wanapoenda kusajili laini zao kuwa makini sana kwa sababu tumebaini kuwa kuna baadhi ya hizi namba zilizosajiliwa ukifuatilia unakuta picha ni mtu tofauti na wengine ni marehemu wakati laini hizo zinaendelea kufanya kazi, tumekamata laini sita ambazo zilikuwa zimesajiliwa kwa kutumia majina ya watu wengine”
Sambamba na hilo amewataka mawakala wanaofanya usajili batili kuacha tabia hizo mara moja huku akiwasihi viongozi wa makampuni ya laini za simu za mkononi hapa nchini kuwaelekeza wateja wao jinsi ya kubaini kama kitambulisho chake au namba yake ya NIDA imetumika kusajili namba asizozifahamu.
0 Comments