Siku hizi mabwana na mabibi Shamba feki wako wengi. Mara oo limeni vanilla kilo shilingi milioniii.
Ni Kweli vanilla kilo ni kati ya 800000-1000000 kwa kilo kwenye Soko la dunia. Eka moja ukiitunza vizuri utapata magunia 5 aka kilo 500. Piga 500 x 1000000 = 500,000,000= aka nusu bilionea.
Sasa yamezuka mijitu yanawashawishi wakulima bila kuwaeleza ili uvune gunia 5 kwa Eka unatakiwa ufanye Nini Na usubiri muda gani toka upande hadi uanze kuingia ubilionea.
Mimi napenda Kilimo. Mimi nimesomea Kilimo (Diploma in Irrigation Engineering na BSc Agriculture Science) kabla sijachepukia fani nyingine. Nina shamba la mpunga Kahe na huku Togo nalima mpunga na vanilla. Nimewahi kuwa Production Manager NAFCO na Mamlaka ya Pamba.
Kwa hiyo Kilimo nakijua.
Ugumu wa vanilla ni huu:
1. Vanila ni kama mtoto wa geti kali. Havumilii shida haswa kiu. Uhakikishe hapati kiu hâta kidogo la sivyo utaambulia patupu. Mtoto si riziki.
2. Mpaka ikomae ianze kutoa gunia 5 kwa eka usibirie kati ya miaka 3-5. Mkulima mnyonge ataweza? Wakulima wetu wanalipa ili ndani ya miezi 3-6 avune chakula na auze ziada. Miaka 6 si atakufa? Atakula kwenu?
3. Vanilla hubeba mimba (pollination) Siku Moja Maalum katika mwaka. Siku hiyo ikipita vanilla haibebi tena mimba. Ili pollination itokee mkulima anahitajika aisaidie vanilla kubeba mimba. Achukue pollen (mbegu) kwenye kikonyo na kuipakaza kwenye kizazi (overy) ya ua la vanilla. Akikosea pollination inaweza isitokee na vanilla isipate mimba. Haitazaa. Acha wakulima hâta mabwana na mabibi Shamba n'a wagani feki Hawajui! Itakuwa wakulima?
4. Kabla hujalima vanilla uandae mnunuzi. Vanilla Sawa mbaazi. Ukiikosa mnunuzi utafanyaje? Kuna wanunuzi wa vanilla. Ongea nao kabla. Huwa biashara inaenda hivi: unaingia Mkataba na mnunuzi. Mnakubaliana utamuuzia kilo ngapi, lini, kwa bei Gani?. Anakuja nusu ya malipo. BAADA ya hapo unaongea na shipping agent. Mnakubaliana gharama za usafirishaji na taratibu za malipo zitakuwaje?
Haya mkulima kolo ataweza?
Wizara iwaelimishe wakulima na iwasaidie kutafuta wauzaji na wasafirishaji. Iwasaidie kipindi wanasubiria vanilla ikomae. Watakatana akiuza. Otherwise acheni kuwasumbua wakulima. Vanillaaaa, vanillaaaa!
Kama rahisi limeni basi muwaonyeshe wakulima mfano?
Ngoja nilale mie asali isinipalie!Mlalahoi Mimi
0 Comments