Mratibu wa Programu ya Utafiti wa Zao la Karanga nchini Kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania TARI kituo cha Naliendele Dkt. Happy Daudi amewahimiza Maafisa Kilimo ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega kuwasaidia wakulima kutatua changamoto za magonjwa mbali mbali na wadudu waharibifu wa zao hilo.
Akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo watalaamu hao alisema kuwa wakulima wanapaswa kuwa na matumizi ya mbegu bora ili kuzalishaji zao hilo kwa tija.
Alisema kuwa Maafisa kilimo wanapaswa kuzifahamu kanuni za Kilimo bora cha zao hilo ili waweze kwenda kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima.
"Mpaka Sasa zipo aina 11 za mbegu bora za karanga ambazo zimefanyiwa utafiti na Tari Naliendele ambazo zina stawi kwenye maeneo ya ukame na maeneo ambayo yanapata mvua kidogo"
"Karanga ina faida nyingi ukitumia mbegu bora unaepuka magonjwa kilimo chenye tija ukipanda mbegu moja unatakiwa upate 10 lakini kwa mbegu bora ni zaidi hivyo kumuongezea mavuno mkulima wa zao hilo" alisema Dkt Happy
Katika mafunzo hayo yaliyofunguliwa na Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika, kwa Niaba ya MKurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Said Shemahonge ameishukuru TARI Naliendele kwa utoaji wa mafunzo hayo yaliyotolewa kwa Maafisa ugani wa Halmashauri hiyo.
Mafunzo haya ni mazuri yanaenda kuboresha Kilimo cha karanga katika Halmashauri yetu pia yamekuwa na faida kubwa kwakuwa tutapewa mbegu bora zitakazotumiwa na maafisa ugani kwa ajili ya mashamba darasa pamoja na zile za uzalishaji mbegu bora za zao hilo"alisema Shemahonge
0 Comments