Na fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uwekezaji ya UTT AMIS, Simon Migangala amesema kuwa jitahada zinazofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuvutia wawekezaji ndani na nje ya nchi imekua ni kuchocheo kikubwa cha kampuni hiyo kufanya vizuri.
Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Mkutano Mkuu wa Kampuni hiyo ambapo pamoja na mambo mengine itahusisha taarifa za mifuko sita inayosimamiwa na UTT AMIS huku akisema ukuaji wa mifuko hiyo ni mkubwa.
"Katika taasisi ambazo zimenufaika na jitihada za Rais Samia za kuchochea uwekezaji na sisi UTT AMIS ni mojawapi hivyo tunamshukuru sana Rais Samia kwa jitihada zake za kuiunganisha Tanzania na mataifa mengine jambo ambalo limechoche ongezeko la wawekezaji wa ndani na nje ya nchi "amesema Mkurugenzi Migangala.
Amesema kuwa, miongoni mwa mafanikio makubwa yaliopatika katika mfuko huo ni pamoja na utekelezaji wa mpango mkakati wa mwaka 2019 / 2024 katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo .
Aidha amesema faida katika mfuko wa umoja kwa mwaka wa fedha ulioisha Juni 2022 ilikua ni asilimia 12.6 ikilinganishwa na asilimia 16.6 ya mwaka 2021, kupungua wa faida ya mwaka kulichangiwa na kushuka kwa viwango vya riba sokoni.
Hata hivyo, amesema mwamko na elimu inayotolewa kwa wananchi kuhusu faida zinazotokana na masoko ya fedha, mazingira mazuri ya uwekezaji yenye utulivu wa soko ndio yanayochochea ukuaji mzuri wa mfuko huo.
Sambamba na hayo amewataka Watanzania kujiunga na mfuko huo kwani kutokana na utulivo wa soko la uwekezaji wanatarajia mfuko huo kwa mwaka ujao kukua zaidi na kuongeza faida kwa wanachama.
Hata hivyo amesema mfuko uliofanya vizuri vizuri kiuwekezaji kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 ni mfuko wa Bond Fund ukifuatiwa na Liquid Fund, Wekeza Maisha na kumalizia na mfuko wa watoto.
Awali, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi UTT AMIS Casmir Kyuko amesema kuwa lengo la kufanya Mkutano huo ni kuwaelezea wawekezaji kuwa wao kama wasimamizi pesa zao zipo salama na kuwafahamisha maendeleo ya mfuko yapoje.
"Leo tutakua na mikutano miwili na kesho miwili na siku ya jumapili tutamaliza na miwili ambapo pia tutaweza kuzungumza na wawekezaji wetu na kuwaelezea maendeleo ya mifuko yetu sita ambayo imefanya vizuri na kwamba wawe mabalozi wazuri wa kuwahamasisha na wenzao waje kuwekeza katika mifuko yetu"amesema Kyuko.







0 Comments