Header Ads Widget

JESHI LA POLISI PWANI LAKAMATA WATUHUMIWA 131.

JESHI la Polisi Mkoani Pwani linawashikilia watu 131 kwa makosa mbalimbali na kuokoa mali zilizokuwa zimeibiwa.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha Kamanda wa Polisi Mkoani humo (ACP) Pius Lutumo alisema kuwa watu hao wamekamatwa  katika kipindi cha Oktoba hadi Novemba mwaka huu.


Lutumo alisema kuwa mali zilizookolewa ni pamoja na gari aina ya Toyota RAV 4 yenye namba za usajili T 619 BMQ, pikipiki 13 za aina mbalimbali, televisheni 19, redio tatu, kompyuta mbili, pampu ya maji, kingamuzi, madirisha ya chuma manne na msumeno wa kukatia miti.


Aidha alitaja vitu vingine kuwa ni mchele, sukari, unga kilogramu 25 kila moja, ng'ombe 51, mbuzi 72, kondoo watano, dawa za kulevya aina ya heroin kete 135, bangi kiroba kimoja, puli 147 kete 1,033,  miche 35 ya bangi pombe ya Moshi lita 139 na mitambo mitano.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI