Header Ads Widget

WIZARA YA ARDHI YAONGEZA SIKU, KUSIKILIZA MALALAMIKO YA MIGOGORO YA ARDHI DODOMA

Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam

Wizara ya Ardhi Nyumba,  na Maendeleo ya Makazi imeongeza siku za kusikiliza malalamiko ya migogoro ya Ardhi katika mkoa wa Dodoma baada ya siku tano za mwanzo kumalizika iikiwa kuna ongezeko kubwa la wananchi ambao hawajafikiwa.


Hayo yamezungumzwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Allan Kijazi 

amesema zoezi hilo limeongezewa siku tatu kwa Dodoma hii ni kutokana na malalamiko mengi na wananchi baadhi bado hawajasikilizwa.


Aidha,amesema pia wameona kwamba kuna haja ya wataalamu wao kabla ya kutoa mrejesho kwa badhi ya malalamiko wapate muda wa kufanya uchambuzi wa malalamiko ambayo yametolewa yafanyiwe uchambuzi.


"Hii itatusaidia kuweza kutatua migogoro kwa njia ya haki kwa kila mmoja bila ya kuwa na upendeleo wa aina yeyote na baada ya kumaliza maeneo ya Dodoma tunaendelea na zoezi katika mikoa mingine" amesema Kijazi.


Aidha, kwa upande wa upande wa Dar es salaam walipokea malalamiko 386 uchambuzi wa kina ulifanyika baadhi ya malalamiko yalishatolewa uamuzi na mengine yanaendelea kuchambuliwa katika nyaraka mbalimbali katika kumbukumbu zao ili kujiridhisha kabla ya kutoa maamuzi.


"Kwa wale wananchi ambao bado hawajapata mrejesho wasifikirie kwamba malalamiko yao hayakufanyiwa kazi  yapo maeneo ambayo tulilazimika kukutanisha watu kama yanahusu pande mbili au tatu tukutanishe ili kuweza kusikiliza hoja ili tuweze kutoa maamuzi sahihi" amesema Kijazi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI