Header Ads Widget

WAZAZI WATAKIWA KUFICHUA VITENDO VYA UKATILI

Goodchance Msangi Mwanasheria kutoka Manispaa ya Kinondoni akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi katika uzinduzi wa kampeni ya hatua kwa hatua na mama iliyoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi Kata ya Mzimuni

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Mzimuni Amour Seif Abdalla akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani mara baada ya kuzinduliwa kampeni ya hatua kwa hatua na mama iliyoandaliwa na Jumuiya hiyo

                    xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam 

Wazazi na walezi wameshauriwa kuvifichua vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyofanyiwa watoto wao huku wakitakiwa wazazi hao kuwalea watoto wao katika maadili mazuri sambamba na kuwapatia malezi bora ya hekima na busara Ili waweze kutimiza ndoto zao.


Rai hiyo, imetolewa jijini Dar es Salaam na Mwanasheria kutoka ofisi ya Wilaya kinondoni Goodchance Msangi alipokua akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo, Godwin Gondwe kwenye uzinduzi wa kampeni ya Hatua kwa hatua na mama iliyoandaliwa na Jumuiya wa wazazi Kata ya Mzimuni .


Amesema kuwa, watoto wamekua wakifanyiwa vitendo vya ukatili na watu wa karibu na wanaowaamini, hivyo amewaasa wananchi kuungana pamoja katika kupinga vitendo vya ukatili kwa watoto kwa maslahi mapana ya kumjengea mtoto ustawi uliokuwa bora katika maisha yao.


Aidha, ameipongeza Jumuiya ya wazazi kwa kuzindua kampeni hiyo sambamba na kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa wanafunzi wenye mahitaji wakiwemo mayatima ambapo lengo kubwa la kampeni hiyo ni kuyasemea mema na mazuri yaliofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na kuzitangaza juhudi zinazofanywa ili kuhakikisha Tanzania inapiga hatua.


"Nichukue fursa hii kuwapongeza sana kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya yetu, mmefanya jambo kubwa na zuri la kuigwa na kuisaidia Serikali katika vipaumbele vyake, Serikali imetangaza elimu bure lakini nyie mmekuja kugawa vifaa mbalimbali kwa wananchi Ili kuunga mkono juhudi za Rais Samia "amesema Msangi.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Mzimuni, Amour Seif Abdala ambae pia ni Mwanzilishi wa kampeni ya hatua kwa hatua na mama amesema kuwa kampeni hiyo ni endelevu  wameanza kutoa msaada katika shule tatu, ikiwemo shule ya msingi mzimuni na mikumi pamoja na Sekondari Mzimuni.


Amesema kuwa, lengo la kampeni hiyo ni kuunga mkono jitihada za Rais Samia ikiwa ni pamoja na kuyasemea yale yote yaliofanywa ikiwemo miradi ya maendeleo na kimkakati huku akiahidi kufikia maeneo mengi kuyatangaza  


"Jambo ambalo tumelifanya leo ni kuunga mkono Serikali ya awamu ya sita, wametangaza elimu bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha sita lakini kuna familia duni, mayatima hawana uwezo kwa kujinunulia vifaa vya shule ndio maana msaada huu tumeutoa kwa ajili yao, ili waweze kuendelea na safari yao kutimiza ndoto zao"amesema Amour.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI