Na Gabriel Kilamlya, Njombe
Wakati wahitimu wa darasa la saba kwa mwaka huu wakirejea nyumbani baada ya kumaliza masomo yao ya elimu ya msingi jamii pamoja na wazazi wametakiwa kuwawekea ulinzi na usalama wa kutosha ili wasikutane na changamoto ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia huku wakijiandaa na masomo ya hatua inayofuata.
Afisa elimu kata ya Ramadhani Mwalimu Fortunatus Mbiro ametoa kauli hiyo wakati wa mahafali ya 21 ya shule ya msingi Livingstone iliyopo kibena Mjini Njombe ambapo amesema kwa kuwa kazi ya kumtengeneza mtoto ni kubwa na ni ngumu hivyo ni lazima kuwaheshimu sana walimu ambao kazi zao hazionekani mara nyingi huku akitaka kuendelea kukabiliana na ukatili unaofanyika dhidi ya watoto.
Naibu Mkurugenzi wa shule hiyo Agnetha Mpangile amesema kuondoka kwa wanafunzi hao kusiwe chanzo Cha matatizo mitaani kwani ulimwengu wa sasa unahitaji kujitunza.
Kwa niaba ya wahitimu wa shule hiyo mtoto Gladness Mtokambali wenyewe Wamekiri kupatiwa elimu ya majanga mbalimbali likiwemo la Ukimwi.
Mgeni wa heshima katika mahafali hayo toka kampuni ya Miwati TANWAT bwana Victorino Mhapa yeye anatumia fursa hiyo kuwataka wazazi kuachana na tabia ya kuwapeleka watoto hao kwenda kufanya kazi za ndani badala ya kuwaendeleza kielimu.

0 Comments