Alisema kuwa wazazi hao badala ya kuwaendeleza watoto wao wamekuwa wakifanya anasa huku wakiwa hawatoi huduma za watoto hivyo kukosa mahitaji muhimu ya kielimu.
Aidha alisema kuwa baadhi ya watoto wamekuwa wakijiunga na makundi ya kihalifu kutokana na kutosimamiwa ikiwa ni pamoja na kutopelekwa shule hivyo watoto hao wakijikuta wanaingia kwenye uhalifu.
Kwa upande wake Meneja wa shule hiyo Nuru Mfinanga alisema kuwa wazazi wasiwaingize kwenye migogoro ya kifamilia watoto wao kwani husababisha kuathirika kisaikolojia.
Mfinanga alisema kuwa watoto wanapoingizwa kwenye migogoro ya kifamilia hawawezi kufanya vizuri kwenye masomo yao kwani hawana uwezo wa kichanganua mambo ambapo shule ya Kips kwa miaka mitano imekuwa ikiongoza Wilayani Kibaha.
Kwa upande wa wanafunzi wa shule hiyo Herieth Kapinga alisema kuwa wamefanya vizuri mitihani yao ya kumaliza elimu ya Msingi wanaamini ufaulu wao utakuwa mzuri kutokana na kuandaliwa mazingira mazuri ya usomaji.
Naye mwakilishi wa wazazi Marietha Mndolwa alisema kuwa wazazi wasiwaachie walimu mzigo wa kuwalea watoto badala yake wawe na ushirikiano. Jumla ya wanafunzi 105 wa shule hizo walikabidhiwa vyeti vya kuhitimu darasa la saba
0 Comments