Header Ads Widget

WAFANYABIASHARA MKOANI PWANI WAUNGANA NA KIKWETE JUU YA KUZALISHA BIDHAA BORA



 WAFANYABIASHARA Mkoani Pwani wameungana na ushauri uliotolewa na Rais wa awamu ya nne Dk Jakaya Kikwete kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kushindana na zile zinazotoka nje.


Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Kibaha wakati wa maonyesho ya tatu ya biashara na uwekezaji mkoa wa Pwani mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Mkoa wa Pwani Abdala Ndauka alisema ushauri waliopewa na Rais mstaafu Kikwete wataufanyia kazi.


Ndauka alisema kuwa wanaishukuru serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya kufanyia biashara hivyo watahakikisha wanakwenda na wakati kwa kupata mashine za kisasa ili bidhaa zao ziwe na ubora.


"Ushauri uliotolewa na Kikwete wakati akifungua maonyesho haya ya biashara na uwekezaji alitaka tuzalishe kwa ubora na si kutaka huruma ya serikali kuwapa nafasi wazalishaji bidhaa wa ndani bali wapambane na soko kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora," alisema Ndauka. 


Naye Mwenyekiti wa JWT Taifa Hamis Lihembe alisema kuwa maonyesho hayo yanakuza na kutangaza Masoko na fursa za uwekezaji  na kupata maeneo ya uwekezaji.


Lipembe alisema kuwa wanachama wengi wameitikia kushiriki maonyesho ambapo walizoea ya Dar es Salaam ya kimataifa na mataifa toka nje bidhaa za ndani hivyo itakuza wazalishaji na zitaingia sokoni.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI