Header Ads Widget

RAIS SAMIA KUANZA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU NNE MKOANI KIGOMA.

 


Na Editha Karlo,Kigoma

Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Kigoma.


Akiongea na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Mhe Rais Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema Mhe Rais ataanza ziara tarehe 16 hadi tarehe 19,atapokelewa Wilaya ya Kakonko majira ya saa 4 asubuhi atatembelea Wilaya zote.


Andengenye amesema kuwa Rais akiwa Mkoani Kigoma atafungua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya afya,maji,barabara na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo ya Mkoani  Kigoma.


Alisema pia Mhe Rais atapata  fursa ya kuzungumza na wananchi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya atakazopita.


“Hii ni ziara yake ya kwanza Mkoani kwetu tangy aingie madarakani hivyo ni faraja kubwa wanakigoma kumpokea Rais wetu hivyo niwaombe wananchi wa Mkoa wa Kigoma tujitokeze kwa wingi kumpokea na kumlaki kiongozi wetu wa Kitaifa katika maeneo mbalimbali ambayo atatembelea na kuzungumza na wananchi”Alisema Andengenye

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI