Header Ads Widget

Viongozi wa Jeshi la Polisi watakiwa kusimamia Maadili na Uwadilifu

 


Na Thabit Madai, Zanzibar – MATUKIO DAIMA APP

 

KAMISHINA wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad amewataka Viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazin Pemba kusimamia Maadili, Nidhamu, haki na Uweledi kwa askari wanapotekeleza Majukumu yao ya Kila Siku.

 

Wito huo ameutoa leo wakati wa ziara maalumu katika Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo amepata fursa ya kuzungumza na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo.

 

Kamshna Hamad alisema hatua hiyo ya Viongozi wa Jeshi la Polisi kusimamia vyema Maadili, Nidhamu, haki na Uweledi kwa askari itasaidia kutoa huduma zilizobora kwa jamii.

 


“Jamii inategemea kupata huduma zilizobora kwa Jeshi la Polisi hivyo ni vyema kwenu Viongozi kusimamia Maadili,Nidhamu, haki na Uweledi kwa maafisa wenu,” alieleza.

 

Aidha Kamishna huyo aliwataka maafisa wa Jeshi la Polisi Mkoani humo kila mmoja atimize wajibu wake na kuacha kufanya kimazoea.


 

“Kila Mmoja anapaswa kutimiza wajibu wake ipasavyo na kuacha kufanya kazi kwa mazoea pamoja na kutumia vibaya madaraka waliyopewa,”Alisema.

 

Katika Hatua nyingine alisema, hatosita kuwachukulia hatua za kinidhamu kwa askari atakae fanya kazi kwa kinyume na Utaratibu wa Jeshi hilo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI