Na Pamela Mollel,Arusha
Viongozi wa dini mbalimbali hapa nchini wametakiwa kuendelea kutoa mafundisho mema kwa waumini wao ili kubadilisha tabia mbaya inayopelekea ongezeko la matukio ya kutisha katika jamii
Rai hiyo ilitolewa hivi karibuni jijini Arusha na Shekhe Mkuu wa Msikiti wa Shia Maulid Sombi wakati wa sherehe ya Maulidi
Shekhe Sombi alisema kuwa ni jukumu la kila kiongozi wa dini kutoa mafundisho kwa jamii ili iweze kubadilika na kuwa na tabia inayokubalika katika jamii
"Matukio ya kutisha yapo mengi sanaaa utasikia matukio ya kuuana,kujinyonga,wizi,uchochezi na mambo mengi"alisema Sombi
Alisema vitendo vinavyofanyika havifai hata mbele za Mungu ambapo ameitaka jamii kumrudia Mungu
Aidha alisema kuwa lengo la sherehe hiyo ni Amani mshikamano na upendo huku wakiendelea kudumisha ibada bila kubaguana
0 Comments