NA THABIT MADAI,ZANZIBAR- MATUKIO DAIMA APP
KATIKA Kuhakikisha huduma za mtandao wa simu ya Tigo Zantel unaimarika zaidi kwa wateja, Viongozi wa kampuni hiyo imepita katika vijiji mbalimbali kutoa elimu juu ya huduma zao zinavyopatikana.
Akizungumza katika kijiji cha paje ikiwa ni wiki ya huduma kwa wateja, Mkurugenzi wa kanda ya Zanzibar, Azizi Said Ali, alisema, kampuni yao imejipanga kuona huduma za Tigo Zantel zinaboreshwa ambapo wamekuwa wakipita sehemu mbalimbali kuona changamoto zinazowakabili wateja wao wanazitatua kwa wakati.
Alisema, mara baada ya kusikiliza changamoto hizo watazifanyia kazi ili huduma ziweze kupatikana kwa uhakika kupitia mitandao yao.
Alisema, imani yao itawafikia wateja wao wengi ambapo tokea kuanza wiki wamekuwa wakiwapitia wateja wao kuona changamoto gani zitawakabili.
Hata hivyo, alisema huduma hazijapungua isipokuwa uhamisho uliofanyika katika zantel kupeleka tigo ndio imefanya kuwepo kwa changamoto hiyo.
Hivyo, aliwaomba wananchi kuendelea kutumia huduma zao kwani sasa hivi mteja wa tigo amekuwa akilipia huduma mbalimbali za serikali ambapo awali alikuwa hawezi kutumia huduma hiyo kupitia line ya tigo pekee.
Nao wananchi walisema licha ya kuwepo kwa changamoto katika mitandao hiyo lakini kinachowapendeza ni uongozi wa kampuni hiyo wamekuwa wakipita kila sehemu kusikiliza changamoto na kuweza kuzitafua.
Hivyo, waliuomba uongozi wa kampuni hiyo kuboresha zaidi huduma ili kuona wanafaidika na huduma wanazozitoa
Kwa upande wao Wananchi waliopitiwa na huduma hizo Wamepongeza Kampuni hiyo kwa kuona haja ya kuwafikia walipo.
"Kitendo walichokifanya ni kitendo cha Kiungwana kabisa ambapo wamekuja kutusikiliza kero zetu zinazotukabili," alisema mmoja aliejitambulisha kwa jina Salim Juma Mkazi wa Paje.
0 Comments