Taswira
ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Mkoani Dodoma itakavyoonekana
mara baada ya kukamilika kwa Ujenzi wake ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la Msingi la mradi huo Mkubwa
nchini.
Katika
Awamu ya kwanza, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato utakuwa na uwezo wa
kuhudumia Ndege kubwa aina ya Dreamliner 787 yenye uwezo wa kubeba
abiria 350. Aidha, uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 1.5
kwa mwaka na utakuwa na miundo mbinu mbalimbali kama mnara wa kuongozea Ndege,
Jengo la Watu Mashuhuri, jengo la Zimamoto, mizigo, Jengo la Rais, pamoja na
Karakana.
Mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
Msalato Mkoani Dodoma unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2024.
0 Comments