Header Ads Widget

TANZANIA YA AMANI YAWA KIVUTIO CHA WAWEKEZAJI


Na Teddy Kilanga,Matukio DaimaAPP,Arusha.

Serikali  imewaalika wawekezaji kuja kuwekeza nchini kwenye sekta ya utalii, kwa sababu ni nchi yenye amani na utulivu na watu wenye ukarimu.

Akizungumza jijini Arusha kwa niaba ya Rais Samia Hassan Suluhu,  Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa wakati akifungua mkutano wa 65 wa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) Kamisheni ya Afrika, alisema  Tanzania ni nchi yenye vivutio vingi na maeneo mengi hivyo kuja kwa wawekezaji nchini kutakuwa na fursa zaidi nchini.

Aidha amepongeza uamuzi wa Katibu Mkuu Mtendaji wa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) na washiriki wake kuunga jitihada za Tanzania kutunza mazingira kwa  kupanda miti baada ya mkutano huo .


Alisema uamuzi wa UNWTO kuipa Tanzania mwenyeji wa mkutano huo ni sahihi na umekuja wakati muafaka ambao nchi ina rasilimali nyingi za utalii ambazo wamekaribishwa kuzitembelea na kufurahi. 


Alisema  kabla ya janga la Uviko-19 kuingia nchini mwaka 2019 Tanzania iliingiza dola za Kimarekani bilioni 2.6 zilizotokana na sekta ya utalii na kuchangia ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja milioni 1.5

Aidha alisema kwa mwaka 2022 takwimu zinaonyesha  sekta ya utalii inabidi kuimarika zaidi hususani baada ya uzinduzi wa programu maalum ya Rais Samia Hassan Suluhu ya The Royal Tour ambapo mapato yatokanayo na utalii yameongezeka kwa asilimia 81.8 kutoka Dola za Kimarekeni milioni 714.59 mwaka 2020 na kufikia Dola za Kimarekani bilioni 1.3 mwaka 2021.

Pia alisema Tanzania baada ya janga hilo ikiendelea kufanya jitihada mbalimbali za kufufua sekta ya utalii, ikiwemo utengenezaji wa Filamu ya The Royal Tour iliyoongeza mapato  na watalii nchini.

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Pindi Chana alisema mkutano huo umehudhuriwa na waziri zaidi ya 33 kutoka nchi wanachama  wa UNWTO  ukanda wa Afrika mwenye dhamana ya utalii masuala ya Utalii na Mali

Alisema mkutano huo utajadili masuala mbalimbali ikiwemo mstakabali wabustawi wa Maendeleo ya sekta ya utalii barani Afrika haswa baada ya athari  za UVIKO 19  uliokuwa umeathiri sekta ya utalii Kimataifa kwa wastani wa asilimia 50 hadi 85 katika nchi mbalimbali ikiwemo  Tanzania.

Alisema mkutano huo pia utahusisha wadau mbalimbali wakiwemo wataalam wabobezi  wa utalii kwenye vitengo vya ukarimu katika ngazi ya kimataifa na kikanda,watoa huduma  mbalimbali katika mnyororo wa utalii,uwekezaji pamoja na watu mashuhuri zaidi ya 50"

"Lengo la ujio wa wabobezi hawa waliobobea katika sekta ya utalii ni kuwapa semena wadau wa sekta ya utalii hapa nchini katika masuala yote muhimu yanayohusu sekta hiyo kuanzia kwenye masoko,fursa, ukarimu pamoja na mwenendo mzima wa kukuza sekta hiyo hapa nchini".

Kwamujibu wa  Balozi Pindi alisema mkutano huo utawajengea uwezo wadau wa sekta ya utalii hapa nchini katika kutangaza utalii,kuendeleza na kufungamanisha mazao ya utalii katika kanda mbalimbali za utalii za utalii nchini kulingana na shabaha ya nchi kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni tano ifikapo mwaka 2025 na pato la Taifa  Dolla za Kimarekani Bilioni sita. 

"Mkutano huu ni matokeo ya amani na ultulivu tulionao tangu nchi yetu ilipopata uhuru na ndiyo sababu mwaka jana katika mkutano wetu kama huu uliofanya nchini Cape Vade wajumbe kwa pamoja waliridhia mkutano huo kuja nchini.


Mkutano huo umeenda sambamba na  kauli mbiu ya "Kujenga upya  ustahimilivu  wa utalii  wa Afrika Afrika ajili a maendeleo jumuishi ya kijamii na kiuchumi,"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS