Mkurugenzi wa Ilemela English Medium Primary School David Maduhu ameiomba Wizara ya Elimu kuthamini shule za binafsi kama inavyothamini shule za serikali kutokana na kuzichukulia kama za upinzani huku ukizingatia shule hizo zimekuwa zikiongoza katika matokeo ya mitahani yoyote
Mwalimu mkuu wa Ilemela English Medium Primary School Sande Jackson wazazi wanaosomesha watoto katika shule hiyo kutoa ushirikiano wa kushiriki makambi ya masomo katika shule hiyo ili kuwaongezea ufanisi wa kufanya vizuri katika masomo pamoja na mitihani.
Ilemela English Medium Primary School imepanda kitaaluma mwaka jana na kupata alama A katika matokeo ya mtihani wa Taifa na katika mitihani ya Kata ,wilaya na mkoa imeshika nafasi ya 3 na kupata wastani wa A kwa mitihani yote na mwaka huu wanatarajia kushika nafasi ya 10 bora kitaifa.
0 Comments