Header Ads Widget

MBUNGE BENAYA KAPINGA AWATAKA WAZAZI KUZINGATIA VIPAJI VYA WATOTO WAO

 


Na Amon Mtega,Mbinga.

MBUNGE wa Jimbo la Mbinga Vijijini Mkoani Ruvuma Benaya Kapinga amewataka Wazazi na Walezi waviendeleze vipaji vya watoto wao kwa kuwa vipaji hivyo huwawezesha watoto kuwa sehemu ya ajira na kupunguza tatizo la ajira ambalo limekuwa ni changamoto kutoka na ushindani uliopo.


 Kapinga ametoa wito huo  wakati akihutubia kwenye mahafali ya kidato cha nne yenye wahitimu 73  katika Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Luise iliopo kata ya Maguu Wilaya ya Mbinga Mkoani humo ambapo mahafali hayo yameambana na harambee ya kuchangia ujenzi wa uwigo wa shule hiyo huku Mbunge huyo amechangia mifuko 100 ya Saruji.


 Mbunge Benaya ambaye amekuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo amesema kuwa watoto wetu wamekuwa na vipaji mbalimbali ambavyo vikiendelezwa vitasaidia kuwa sehemu ya ajira hivyo Wazazi na Walezi wanapaswa kuviendeleza na siyo kuvidumaza kwa kuvibeza.

 

 Hata hivyo Mbunge huyo amezipongeza taasisi za kidini kuwa zimekuwa zikifanya kazi ya kuhudumia jamii katika sekta mbalimbali ikiwemo ya Elimu na Afya jambo ambalo imekuwa msaada mkubwa kwa jamiii.


Awali mwanafunzi Doris Haule akisoma risala mbele ya mgeni rasmi huyo amesema kuwa Shule hiyo ya wasichana yenye kidato cha kwanza hadi cha sita na inamilikiwa na watawa (Sisters)wa Mtakatifu Vincent  Paul Mbinga imeanza mwaka 1991 ikiwa na wanafunzi 70 hadi sasa ina wanafunzi 345 huku walimu wakiwa 20 na watumishi wa idara zingine 15.


 Mwanafunzi Doris amefafanua kuwa tangu kuanzishwa kwa shule hiyo ufaulu umekuwa ni waasilimia 100 hadi sasa jambo ambalo imeifanya shule hiyo kutambulika katika maeneo mbalimbali ya Nchini.


 Aidha Doris amezungumzia baadhi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo kuwa ni ukosefu wa wigo ambao utawasaidia kuimarisha ulinzi wa kutokuingiliwa na baadhi ya watu wasiyokuwa na nia njema.


 Naye mkuu wa shule hiyo mtawa Mariapia Kayombo wakati akimkaribisha Mbunge huyo amesema kuwa anawashukuru Wazazi na Walezi kwa kushirikiana kahakikisha watoto wanapatiwa mahitaji ya shule na hatimaye kuwafanikishia kuhitimu elimu yao vema.


 Mkuu huyo amesema kuwa licha ya kumudu watoto kufanya vizuri katika masomo yao lakini wamekuwa wakifundishwa na masomo ya stadi za kazi kwa vitendo ili kuwajengea uwezo wa kujitegemea.

                             Wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya Mtakatifu Luise 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI