Na Amon Mtega, Mbinga.
MJUMBE wa Kamati ya utekelezaji wa baraza la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi CCM Tanzania (UWT) Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma Theresia Kapinga amekipongeza Chama hicho Wilayani humo kwa kuyajali makundi maalumu (Walemavu)kwa kuwapa nafasi mbalimbali za uongozi.
Kapinga ambaye ni mlemavu wa miguu amesema kuwa CCM Wilaya ya Mbinga kupitia katibu wa Chama hicho aliyehamishiwa Kinondoni Dare-eslaam Jacob Siay kimejenga misingi ya kuhakikisha makundi maalumu yanapatiwa vipaumbele jambo ambalo limewafanya watu wenye ulemavu katika chaguzi hizi kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kisha kupigiwa kura na Wajumbe.
Mjumbe huyo ambaye amewahi kugombea nafasi ya ubunge kupitia makundi maalumu ya uwakilishi amesema kuwa alifika hadi ngazi ya Taifa kura hazikutosha alibahatika mwingine na kuwa ataendelea kuomba nafasi za uwakilishi ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM na kwenye taasisi mbalimbali.
Akimtaja katibu wa Chama hicho aliyewahi kufanyia kazi Mbinga kisha kuhamishiwa Jijini Dar-es-salaam Jacob Siay amesema kuwa ni moja ya katibu waliofanya kazi kubwa ndani ya Wilaya hiyo kwa muda mfupi na kukiimarisha Chama kuwa pamoja na kila mmoja wakiwemo Walemavu kupatiwa haki ya kugombea nafasi za uongozi.
Amefafanua kuwa katibu huyo alimuita ofisini wakati mchakato wa uchukuaji wa fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ngazi za matawi,kata, na Wilaya kwenye Chama na Jumuiya zake ,akapatiwa maagizo na katibu huyo kuwa ahakikishe anawahamasisha Walemavu wenzake kuwania nafasi hizo jambo ambalo adai amelifanya na baadhi yao wamebahatika kuchaguliwa akiwemo yeye.
Hata hivyo Kapinga ambaye pia amewania nafasi za uongozi ngazi ya mkoa kwenye Chama cha CCM amempongeza mwenyekiti wa Chama hicho Taifa ambaye pia ni Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwa ni moja ya kiongozi ambaye yupo karibu na makundi maalumu.
0 Comments