Header Ads Widget

MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA AISHUKURU TARI

 

Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga Mhandisi  Charles Masondya ameishukuru Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania TARI kupitia Kituo chake cha Uyole Mbeya na Tumbi Tabora  kwa kuendeleza tafiti za magugu chawi (Striga/Kiduha) kwenye mazao ya ulezi, mtama, mahindi na uwele  katika wilaya hiyo.


Mhandisi  Masondya ameyasema hayo ofisini kwake leo mjini Igunga alipotembelewa na watafiti kutoka TARI  walioenda kujitambulisha na kuanza majaribio mapya.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo cha Utafiti wa Kilimo cha TARI Uyole Dkt. Dennis Tippe amesema  kuwa katika kutanua wigo wa utafiti na mashirikiano na vyuo vikuu vya nje. Timu hiyo ya TARI Uyole imembatana na Dkt. Jamil Muhammad wa Chuo Kikuu cha Sayansi cha Mfalme Abdullah cha Saudi Arabia (King Abdullah University of Science and Technology). Wapo mkoa wa Tabora ili kushirikiana katika utafiti wa kutokomeza tatizo la Striga (Kiduha) katika mazao ya nafaka.











Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI