Header Ads Widget

MKURUGENZI MANISPAA YA SONGEA AWAKEMEA WAKUU WA IDARA YA ELIMU TABIA YA KUWANYANYASA WALIMU

 







Na Amon Mtega_ Matukio Daima APP-Songea.


MKURUGENZI wa Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma Dkt Frederick Sagamiko amewataka wakuu wa idara kitengo cha Elimu pamoja na walimu wakuu wa Sekondari na Msingi kuacha kutumia lugha za kejeli kwa baadhi ya walimu wanaohitaji kutatuliwa changamoto za kikazi.


Dkt Sagamiko ametoa wito huo wakati akifungua mkutano mkuu wa nusu muhula wa Chama cha Walimu (CWT) Manispaa ya Songea ambapo mkutano huo umehudhuriwa na wawakilishi 108 kutoka kwenye matawi yao.


Sagamiko ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo amesema kuwa kunatabia imejengeka kwa baadhi ya wakuu wa idara ya Elimu kutumia lugha ambazo siyo rafiki kwa Walimu ambao huomba watatuliwe shida zao jambo ambalo amesema kuanzia sasa likome lisijirudie tena.



Mkurugenzi huyo amesema amesomewa risala ya walimu bado kunaeneo la baadhi ya wakuu wa Shule kuwanyanyasa walimu ambao ni wawakilishi kwenye maeneo yao ya kazi kwa kuwanyima ruhusa ya kwenda kwenye mikutano ya uwakilishi jambo ambalo halitakiwi.


 Aidha amezungumzia baadhi ya changamoto ambazo zimeainishwa kwenye risala hiyo ikiwemo ya baadhi ya wanachama CWT kuondolewa kwenye makato ya ada ya uanachama ya asilimia mbili bila utaratibu kuwa ataenda kulishughulikia ili kuwabaini waliofanya jambo hilo.


Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Walimu CWT Manispaa ya Songea Mkoani humo Emmanuel Komba amesema kuwa licha ya Walimu wengi zaidi ya 400  kupandishwa madaraja lakini bado kumekuwepo na baadhi ya changamoto kama kutokuwepo kwa Elimu sahihi juu ya Kikokotoo , baadhi ya Walimu wengi kutopatiwa stahiki za mwajiri wao pindi wanapopatiwa matibu.





Mwenyekiti Komba licha ya kuzitaja changamoto hizo lakini bado amempongeza mkurugenzi huyo pamoja na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuzungumza kero za Walimu ikiwemo ujenzi wa miundombinu kama madarasa zaidi ya 76 yamejengwa ndani ya Manispaa ya Songea jambo ambalo limewapunguzia adhaa kwa Walimu katika maeneo yao ya kazi.


 Aidha awali akisoma risala katibu wa Chama cha Walimu Manispaa ya Songea Benardi Mbawala amesema kuwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi watumishi wanapofanya kazi vema wanastahili kupata tuzo yaani kupandishwa madaraja (Promotion)kwa mujibu wa miongozo inayotolewa na Serikali.

    


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI