Header Ads Widget

WAJASIRIAMALI WADOGO NA WASIOKUWEPO KWENYE SEKTA ISIYOKUWA RASMI WANUFAIKA NA NSSF

 


Na Rehema Abraham_ Matukio Daima APP- Kilimanjaro


Meneja wa NSSF Mkoa wa Kilimanjaro Large Materu amesema kuwa kwa sasa mfuko huo unatoa mafao mbalimbali  kwa vijana na  wajasiriamali wadogo yakiwemo mafao ya uzee .


Ameyasema hayo  mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro  katika  hafla  uzinduzi wa ofisi za Mkurabita ziliozinduliwa na waziri wa nchi ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa umma na utawala Bora  Mh.Jenista Mhagama.


Amesema kuwa mfuko una jukumu la kuwafikia waajiri lakini pia una jukumu la kuwafikia wale ambao hawapo kwenye secta isiyo Rasmi kwajili ya kujiandikisha na wawe wanachama wanaochangia mfuko wa hifadhi NSSF ili waweze kufaidika na Fursa Mbalimbali zinazopatikana katika mfuko ikiwemo mafao.


"Kwa sasa mfuko tunatoa mafao kwa wajasiriamali na tuna mafao manne ambayo tayari yameanza kipatikana yakiwemo mafao ya uzee ,pensheni ya urithi , mafao ya uzazi pamoja na msaada wa gharama za mazishi ,hayo ni mafao ambaayo tunatoa kwa wajasiriamali wa Tanzania waliojiajiri wenyewe katika sekta isiyokuwa Rasmi Alisema" Materu.


Amesema kuwa Nia na lengo ni kuhakikisha kuwa watanzania hao wanaendelea kufanya shughili zao huku wakiwa ndani ya hifadhi ya jamii ili pindi wanapopatwa na majanga yeyote mfuko wa jamii uweze kuwasaidia.


"Majanga haya ni Kama uzee ,kifo ,ugonjwa ,kukosa ajira na pia kufiwa haya yote tunasema ni majanga na mtu yanapomfika anahitaji apate msaada kutoka katikaa hifadhi ya jamii ambayo sisi NSSF ndio kazi yetu Kama mfuko" Alisema Materu.


Sambamba na hayo amewataka watanzania kuchukuwa fursa hiyo kwenda katika kituo hicho jumuishi Cha Mkurabita ili waweze kupata elimu ya hifadhi za jamii ili mwisho waweze kuamua kujiandikisha na kuchangia wao wenyewe kwa ihari Yao wenyewe.


Hata hivyo amesema kuwa kwa sasa pensheni sio kwa walioajiriwa pekee Bali ni kwa watu wote walioamua kujiunga na mfuko na akukidhi vigezo ambavyo ambavyo ni muhimu vilivyotajwa kwenye Sheria .


"Lakini sio hivyo tu Kuna mafao ya urithi  tunanajua wanadamu tunaishi na baadae tunakufa na tukifa Kuna watu ambao tunawaacha watu ambao watahitaji msaada wako kwa namna moja ama nyingine kwa hiyo mfuko pia unatoa mafao ya urithi kwa wategemezi   "Alisema


Hata hivyo amesema nia na lengo ya Serikali ni kuhakikisha kuwa Kila mtu anajiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii ili kuondokana na umasikini pindi mtu anapofikia katika umri wa uzee kwani watu hao wanapofikia katika umri wa uzee wanakuwa hawana nguvu Tena za kuweza kujitaftia kipato Chao .


Katika mafao ya uzazi,yanalenga kumsaidia mwanamama aliyepata mtoto ili aweze kujilea mwenyewe na kilea mtoto wake ambapo amesema kuwa mafao hayo mama atapata kabla na baada ya kijifungua.

mwaisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI