Na Scolastica Msewa, Matukio DaimaApp Kibaha
Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Kibaha Mji imeshtukia ujanja wa DAWASA kuchelewesha uhakika wa huduma ya maji katika Machinjio ya mji huo ili waendee kula Asilimia 10 za maboza yanayopeleka maji wakati wa uchinjaji.
Hayo yamebainishwa na kiongozi wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya Mwenyekiti Mpya wa CCM Wilaya ya Kibaha Mji Mwajuma Nyamka wakati walipofika kukagua maendeleo ya Mradi wa maji katika Machinjio ya kisasa ya mji wa Kibaha iliyopo katika Kata ya Pangani.
Kero hiyo ilichangiwa na Wajumbe tofauti tofauti wa Kamati hiyo ya Siasa ya CCM ya Kibaha Mji ambapo wote walionesha kukerwa na tatizo hilo la ukosefu wa huduma ya uhakika ya maji baada ya DAWASA Kibaha kuonesha kukosa jibu la uhakika la lini huduma hiyo ya maji itapatikana katika mabomba badala ya kuletewa maji na Mamlaka hiyo kwa maboza.
"Kuna yanayozungumzwa kwamba mnachelewesha kukamilika kwa mradi huu wa maji ili muendelee kupata asilimia kumi ya kuleta maboza hapa hilo ndio jambo lipo" alisema Nyamka.
Nyamka alisema ukosefu wa uhakika wa huduma ya maji safi ya bomba katika Machinjio hayo ni kuhatarisha maisha kwa walaji wa nyama kutoka mjini huo wa Kibaha na Wilaya zingine zinazotegemea kupata nyama kutoka Katika Machinjio hayo.
"Machinjio hii inatakiwa ifanye kazi na hapa wanachinja kule ni chakula cha binadamu wanakula watu wa Kibaha na nje ya Kibaha wanakula nyama zinazotoka hapa tutakaa tu tusubirie majibu yenu mtakayo leta mezani kwa muda mnaoutaka kwenye karatasi?" Alihoji Nyamaka baada ya DAWASA kusema watawapelekea Kamati hiyo majibu mezani kwamba lini huduma ya maji ya uhakika itafikishwa Machinjioni hapo.
"Kulikuwa hakuna haja ya kuja huku kukagua mradi tungekaa ofisini kusubiri tuletewe taarifa ya mradi ofisini lakini wamefika eneo la mradi ili wajionee maendeleo ya Mradi pamoja na wapewe majibu sahihi ya maendeleo ya Mradi huo hivyo tupewe muda kamili lini huduma ya uhakika ya maji itapatikana katika Machinjio haya" alisema Nyamka.
Awali Akitoa taarifa ya maendeleo ya maendeleo ya Mradi wa maji katika Machinjio ya kisasa ya mji wa Kibaha Kaimu Meneja DAWASA Kibaha Hosea Respicius alisema ukamilishaji wa mradi wa maji huo upo katika hatua ya manunuzi ya vifaa ambapo wanasubiri kuletewa vifaa hivyo Kukihitajika huduma ya maji Machinjioni hapo DAWASA huingia gharama ya kupeleka maboza ya maji ili Wananchi wapate huduma.
Alisema DAWASA wataandaa taarifa ya maendeleo ya Mradi huo watapeleka kwenye kamati hiyo ya Siasa ya CCM Wilaya ili Wasome taarifa kamili, ndipo Wajumbe wakapiga kelele za kupinga maamuzi hayo na ndipo Mwenyekiti huyo wa CCM Wilaya akaanza kuongea kupinga taarifa hiyo.







0 Comments