NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
Mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ametembelea mradi wa uboreshaji umeme unaotekelezwa katika Kijiji cha Boro katika Kata ya Kibosho Kirima Jimbo la Moshi vijijini.
Eneo hilo la Kata ya Kibosho Kirima kulikuwa na shida ya kukatika umeme kwa kipindi kirefu kutokana na umeme kuwa mdogo na wateja kuwa wengi.
Akitembelea mradi huo, Mbunge aliongozana na Meneja wa TANESCO wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Abdulrahman Nyenye ambapo mradi huo umekamilika kwa zaidi ya asilimia 80.
Mbunge amemshukuru Meneja wa Mkoa kwa jinsi ambavyo Serikali imetekeleza ahadi ya kuboresha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika jimbo la Moshi vijijini.
Amemwambia, wana mategemeo makubwa ya ongezeko la umeme pindi mradi huo utakapokamilika ambapo wananchi wanategemea kujiajiri kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya kijamii katika kijiji cha Boro.
0 Comments