Header Ads Widget

MBIO ZA SERENGETI SAFARI MARATHON KUFANYIKA NOVEMBA 12 HIFADHI YA SERENGETI

 


Kocha kutoka marekani Alexander Crowther akizungumza na waandishi

Na Pamela Mollel, MatukioDaimaAPP ,Arusha 

Mbizo maarufu nchini  Serengeti Safari Marathon kufanyika November 12 mwaka huu katika hifadhi ya Serengeti upande wa Ndabaka gate

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha  mratibu wa mbio hizo John Temu alisema mbio hizo hufanyika mara moja kwa mwaka katika hifadhi ya Serengeti 


"Maandalizi  ya tukio hili yamekamilika kwa asilimia kikubwa na tumeweza kuboresha T-shirt,Medali,Kofia na mambo mengine ya msingi"alisema Temu

Mwenyekiti wa chama cha riadha mkoa wa Arusha Gerard Babu akizungumza na waandishi

Alisema watu watakao shiriki katika mbio hizo watapata fursa ya kufanya utalii wa ndani kwa kujionea wanyama katika hifadhi ya Serengeti 


Aidha alisema lengo hasa la kufanya Marathon hiyo nikuhamasisha utalii na michezo hapa nchini jambo ambalo litawapa watu  fursa ya kupenda utalii na michezo 


Aliongeza kuwa mbio hizo zina kilometa 42,kilometa 21,kilometa 10 na kilometa 5


Pia aliongeza kuwa katika kuweka sawa wakimbiaji wamepata bahati ya kumleta kocha wa marekani ambaye kazi yake kubwa ni kuwapa mafunzo kabambe wachezaji wa mbio za ndani na zakimataifa


Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha riadha mkoa wa Arusha Gerard Babu alipongeza waandaaji wa mbio hizo kwa kuwatambua wanariadha chipukizi

Alisema kuwa ujio wa kocha kutoka marekani umekuwa neema kwa wanariadha nchini ambapo kocha huyo aliweza kugawa vifaa kwaajili ya wanariadha 

Diamia Christian na wakimbiaji wengine walimpongeza kocha huyo kwa kugawa viatu na Tshirt kwaajili ya kuhamasisha riadha nchini 

Marathon ya serengeti safari  ilianza mwaka 2018 ikiwa na wakimbiaji 400, kila mwaka ilikuwa ikiongeza idadi ya wakimbiaji ambao 2021 wakimbiaji 1500



Damian Christian mwanariadha


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI