Header Ads Widget

KIWANJA CHA NDEGE CHA KIA KINAMCHANGO MKUBWA KUKUZA UCHUMI WA NCHI




Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma

KAMPUNI ya Uendelezaji na Uendashaji na Kiwanja cha Ndenge cha Kilimanjoro International Airport KADCO imesema kuwa kiwanja hicho cha KIA kinamchango mkubwa wa kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta mtambuka ikiwemo sekta ya utali .


Pia sekta hiyo imekuwa ikitoa usafirishaji wa mazao kutoka sekta ya kilimo na mifugo kwenda katika masoko ya kimataifa ya nje ya nchi.



Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya uendelezaji na uendashaji na kiwanja cha Ndenge cha Kilimanjoro international airport KADCO Christine Mwakatobe aliyasema hayo leo jijini hapa wakati akitoa taarifa ya utendaji wa kampuni hiyo kwa vyombo vya habari .


Alisema kuwa kiwanja hicho cha KIA kinasaidia kukuza sekta mtambuka ikiwemo sekta ya utalii, kilimo pamoja na mifugo kwa kusafirisha mazao ya sekta hizo kwenda katika masoko ya kimataifa.


" Kiwanja Kimekuwa kikikuza sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Utalii, kilimo pamoja na sekta ya mifugo kwa usafirishaji mazao ya yanayotokana na sekta hizo," Alisema Mkurugenzi Mtendaji huyo


Katika hatua nyingine Mwakatobe akatumia fursa hiyo kueleza mipango ya kampuni hiyo ya KADCO kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ikiwemo kuongeza idadi ya abiria kwa asilimia 18 pamoja na kiwango cha mizigo kwa asilimia 16.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI