Header Ads Widget

MALIMA, MADC NENDENI MKASOME MIKATABA YA LISHE MUIELEWE


NA CHAUSIKU SAID, MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adamu Malima amewata Wakuu wa wilaya  kuhakikisha wanasoma na kuielewa mikataba ya lishe ili kuweza kupata matokeo chanya yatakayo saidia kupunguza gharama za matibabu. 


Hayo ameyabainisha katika kikao Cha kusaini mikataba ya lishe na kueleza kuwa Kama watasoma na kuielewa itawasaidia kuweza kufikisha elimu kidogo Kwa wananchi bila kuathiri uchumi.


Malima ameeleza kuwa watu wanapaswa kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu Mtoto ambaye anaathirika na maswala ya lishe ambapo hupelekea uwezo wake wa kutafakari kuathirika Kwa kukosa lishe bora.


"Unakuta Mtoto wa miaka 4-5 anakula asubuhi mchana na usiku ugali huyo ni lazima umkute  ana kitumbo kimetangulia Kwa sababu ya kukosa lishe" Alisema Malima.


Amefafanua kuwa kwenye Mikataba hiyo Jambo moja kubwa ambalo lipo ni elimu ya umma na mawasiliano ya lishe na kufahamu ni namna gani  swala Hilo linamgusa Mtoto kabla ajazaliwa mpaka anapofikisha miaka 5.


" Na lishe sio lazima iwe nyama, maziwa inaweza kuwa ugali dagaa lakini ikawa inamchangayo wa matunda, Kama machungwa n.k" Alisema Malima.


Aidha amefafanua kuwa Madc wanapaswa kutengeneza programu ya lishe itakayowasidia wananchi kuelewa umuhimu wa lishe na kuweza kuwapa elimu kidogo itakayosaidia kufahamu wanayopaswa kuyafanya Kwa watoto.


Kwa upande wake mmoja wa Wakuu wa wilaya ya Magu  Salum Kalli ameeleza kuwa watahakikisha wanatekeleza kile walichoambiwa na kutokuwa kikwazo na badala yake watahakikisha wanasimamia vizuri swala la lishe ipasavyo.


"Tutakwenda kusoma na kuelewa na kufanya utekelezaji na tunakuhakikishia hatutakuangusha kwenye Jambo hili tunakwenda kusimamia ipasavyo" Alisema Kalli.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI