MAHAKAMA ya wilaya ya Iringa Imetaifisha Gari aina ya Scania namba T390 DPM likiwa na tela namba T 301DFH inayosadikiwa kuwa mali ya kampuni ya MAP GROUP kuwa mali ya Serikali yenye thamani ya shilingi zaidi Million 120 na kuwahukumu watuhumiwa wawili waliokutwa na hatia ya kusaidia kusafirisha Raia wa Ethiopia 78.
Watuhumiwa hao Hilary Shari na Vigoros John wamehukumiwa kwenda jela mwaka mmoja au Faiani ya shilingi Million mbili na woote wawili walikubali kosa la kusaidia kusafirisha raia hao wa Ethiopia.
Watuhumiwa hao walitenda kosa Hilo Tareh 8 ya mwez wa 3 Mwaka huu eneo la Kihesa kilolo hapa Manispaa ya Iringa
Akisoma Hukumu Hiyo Hakim Mkazi Mkuu Said Ally Mkasiwa amesema Watuhumiwa wamekutwa na Hatia na Wamekubali kutenda kosa la kusaidia Kusafirisha Raia hao wa Ethiopia 78.
Wahamiaji hao 78 raia wa Ethiopia wakipitia Nchini Kenya waliwekwa katika Kontaina huku juu wakiwa wametoboa matundu ili kuwezesha hewa kupita.
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Iringa Dr.Agnes Luziga amesema walifanya Juhudi zoote kutafuta Kampuni inayomiliki Gari Hilo ikiwepo kwenda Brela hata hivyo Juhudi hizo Zilishindikana.
Hata Hivyo Mahakama iliwapa nafasi ya kujitetea watuhumiwa woote wawili Ambao walikuwa wasaidizi waliiomba Mahakama kupunguza adhabu Kwa Sababu Ni kosa lao la kwanza na Wanafamilia Inawategemea.
Hivyo Mahakama Ikawahukumu kifungo Cha Mwaka mmoja kila mmoja au Faini ya Shilingi Million 2 na Lori Hilo Aina ya Scania kutaifishwa kuwa Mali ya Serikali.
0 Comments