Header Ads Widget

KUKATIKA KWA UMEME YATAJWA KUKWAMISHA MIRADI MIKUBWA YA MAENDELEO


Na Pamela Mollel,Arusha 

Kamati ya kudumu ya Bunge ya kilimo,mifugo na maji imefanya ziara ya kutembea miradi mbalimbali ya maji ya kuboresha huduma ya maji safi na usafi wa mazingira katika jiji la Arusha na Wilaya ya Arumeru 


Katika ziara hiyo wabunge hao walibaini kuwa changamoto kubwa ya kukatika kwa umeme inapelekea miradi mikubwa ya maendeleo kukwama hali inayopelekea wananchi kukosa huduma ya maji kwa wakati 


Akizungumza katika ziara hiyo mwenyekiti  wa kamati ya kudumu ya bunge ya kilimo,mifugo na maji Dkt.Christine Ishengoma alisema kuwa umeme ukikatika inapelekea msukumo wa maji kuwa chini 


 "Baadhi ya maeneo ambayo miradi inatekelezwa ni wilaya ya arumeru (ASUWSDP)  na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (AUWSA),ukiwemo mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya sh.Bilioni 520"alisema Dkt Ishengoma


Alisema Wilaya ya Monduli  hawana maji ya kutosha na wanampango wa kupeleka  maji hadi huko kupitia mradi huo ili kutatua changamoto  ya maji katika eneo hilo.


"Tunamshukuru Rais Samia kwa kuendelea  kutenga fedha nyingi za miradi ya maji ili watu waweze kupata maji safi na salama kila wakati nchini,"Alisema.



Nae Waziri wa maji  Jumaa Aweso  alisema wao kama wizara yenye dhamana wanaendelea kusimamia  na kufatilia kwa ukaribu ili kuhakikisha  adhma ya Rais Samia ya kumtua mwanamama ndoo kichwani inakamilika.


"Utekelezaji  wa miradi  ya maji inategemea na utoaji wa fedha,mradi huu hatukupata changamoto yoyote na sasa upo  asilimia 96.62 ya ukamilishaji.


Ikiwa mahitaji ya maji kwa jiji la Arusha ni lita milioni 109,mradi una uwezo wa kuzalisha lita milioni 200 kwa siku  hivyo maji haya ni toshelevu na yawafikie na maeneo mengine pamoja na wilaya Monduli  ili kutatua changamoto  ya maji katika maeneo  yao. 


Alisema mikakati  ya wizara  ni kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati ili uweze kutimiza adhma ya ifikapo 2025 kwa Arusha iwe imefikia asilimia  100 ya upatikanaji wa maji safi na salama.



Kwa upande wake Mwenyekiti  wa bodi hiyo muhandisi Dkt.Richard Masika ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ulinzi kwa miundombinu  ya maji na pale wanapoona pana uharibifu basi watoe taarifa mapema ili waweze kufanya matengenezo yanayotakiwa.



Mkurugenzi wa mamlaka  ya maji safi na usafi wa mazingira  AUWSA  Justine  Rujomba ametoa shukrani  zake juu ya utendaji wa utekelezaji  wa miradi ya maji  na kuahidi kupokea  maelekezo  yote yaliyotowa na kuyafanyia kazi  hasa lile la kufikisha maji katika maeneo yote ya pembezoni  mwa miji na maeneo jirani yaliyopitiwa na mradi huo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI