Header Ads Widget

MAMA SALMA KIKWETE AUNGURUMA BURUNDI

 


Na Matukio DaimaAPP,Burundi 

Mke wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete, ameiwakilisha Tanzania kwenye mkutano wa  wanawake, wake wa viongozi wa nchi mbalimbali barani Afrika wanaokutana nchini Burundi.

Wake hao wa viongozi wanakutana Mjini Bujumbura kujadili afya na lishe bora kwa wanawake, watoto na vijana balehe. 

Kongamano hilo la wanawake viongonzi limeandaliwa na Ofisi ya mke wa Rais wa Burundi, Angeline Ndayishimiye na kufunguliwa juzi na Makamu wa Rais wa Burundi, Prosper Bazombanza.

Akihutubia kongamano hilo mwanzoni mwa wiki hii, Mama Salma Kikwete alianza hotuba yake kwa salaam kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Mama Kikwete alisema alipopokea tuu mwaliko wa kongamano hilo hakujiuliza mara mbili, aliomba ruhusa na mumewe, Dr. Kikwete na kuruhusiwa kutokana na umuhimu wa kongamano hilo lenye fursa muhimu ya kubadilishana mawazo kwa dhamira njema ya kuboresha afya ya wanawake, watoto na vijana.

Alisema mkutano huo ni muhimu sana katika ustawi wa jamii na ukuaji wa watoto na vijana na kuongeza kuwa kufanyika kwa mkutano huo kunadhihirisha kuwa Burundi imerudi kusimama baada ya kupitia changamoto mbalimbali.

Naye Makamu wa Rais wa Burundi, Prosper Bazombanza alisema kuwa ana matumaini makubwa na maazimio ya kongamano hilo yatapelekea kuwapo kwa mikakati ya kuboresha afya ya wanawake, watoto na vijana. 

"Tunayo matumaini kuwa maazimio mtakayofikia katika mkutano huu yatapelekea kuwapo mikakati ya kuboreshwa kwa afya na lishe kwa wanawake na watoto katika nchi zetu" alisema Bozambanza.

Aidha wake wa viongozi mbalimbali wa Africa wakiongozwa na mwenyeji wao, Angeline Ndayishimiye, Salma Kikwete wa Tanzania, Aisha Buhari wa Nigeria, waliongoza wake wa viongozi wenzao  katika mkutano huo.

Mbali na wake hao wa viongozi,  mkutano huo pia ulihudhuriwa na wajumbe kutoka mashirika ya  Umoja wa Mataifa (UN) yanayohu wanawake na watoto. 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI