Teddy Kilanga MatukioDaima_ App Arusha.
Halmashauri ya jiji la Arusha imekusanya mapato ya ndani zaidi ya sh 7.2 bilioni katika robo ya mwaka 2022/2023 tofauti na 2021/2022 ambapo walikusanya sh.6.2 bilioni sawa na ongezeko la sh.3.2 bilioni.
Akizungumza Oktoba 21,2022 jijini Arusha na Waandishi wa habari ofisini kwake wakati akitoa taarifa ya mapato ya robo ya mwaka 2022/2023, Meya wa jiji la Arusha, Maximilian Iranqhe amesema fedha hizo zimeelekezwa katika miradi ya maendeleo ikiwemo hospitali ya wilaya na ujenzi wa shule pamoja na mikopo ya asilimia 10 kwa ajili ya vijana ,wanawake na watu wenye ulemavu.
"Fedha hii pia tumeipeleka Tarura zaidi ya sh. bilioni mbili kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara jijini hapa,"amesema Iranqhe
Meya huyo alisema kwa upande wa madarasa serikali iliwapatia sh.bilioni mbili kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 100 ikiwa lengo ni kuhakikisha wanafunzi wanaingia kwa pamoja na sio kwa awamu kama ilivyokuwa ikifanyika hapo awali.
Aidha amesema kuwa ujenzi wa madarasa unaendelea vizuri hadi sasa nakudai kuwa changamoto ya uboreshaji wa miundombinu hiyo kila mwaka unatokana na ongezeko la watoto wanaozaliwa.
Hata hivyo amesema kuwa lengo lao ni kuvuka lengo la asimilia 100 katika robo zote za mwaka huo hivyo anawasisitiza wananchi na wataalamu wa halmashauri hiyo kuendelea kutekeleza wajibu wao.
0 Comments