NA CHAUSIKU SAID MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.
Shirika la lnternews limetoa mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi wa dini, maafisa afya kata na watendaji wa kata kwa lengo la kuwapa uelewa juu ya utendaji kazi wa vyombo vya habari pamoja na waandishi.
Mkufunzi kutoka shirika la lnternews Dotto Bulendu amesema kuwa wametoa mafunzo Hayo kutokana na ugumu ambao waandishi wa habari wamekuwa wakikutana nao wanapokwenda kutafuta taarifa.
Bulendu amesema kuwa Kumekuwa na changamoto kutoka kwa watu wanaotoa taarifa kutoka taasisi za kiserikali na zisizokuwa za kiserikali kushindwa kubaini vyombo vya habari vinavyoweza kufikisha ujumbe sehemu husika.
"Unakuta mtu anataka kuzungumzia kampeni ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi msemaji wa ujumbe Kama huo anapelekwa mwaliko kwenye vyombo vya dini kwa namna moja ama nyingine habari Ile haiwezi kutoka kutokana na miiko ya vyombo hivyo na mwisho wa siku wanabaki wanalaumu waandishi wa habari kuwa habari yao haijatoka" Alisema Bulendu.
Kwa upande mwingine amesema kuwa bado Kuna baadhi ya watu hawajafamu namna kufikisha ujumbe wanaopaswa kutoa hivyo hupelekea habari kutoka katika vyombo mbalimbali.
"Ndio maana washiriki wetu wamepitishwa kwenye Sheria ambazo zinawaongoza waandishi wa habari, kwenye maadili pamojanna aina ya vyombo vya habari" Alisema Bulendu.
Kwa upande wao viongozi wa dini mchungaji Jacob Mutash na Sheikh Msabaha Haruna wamesema kuwa wamekuwa wakifanya kazi bila kuwa na uelewa wowote katika tasnia ya habari na namna ya kufanya kazi na vyombo vya habari.
" Na Leo ndio maana Internews wameamua kutuongezea uelewa namna ya kufanya kazi na vyombo vya habari pamoja na waandishi kwa ujumla" walisema.
Wamesema kuwa kutokana na kukosa uelewa juu tasnia ya habari watu wengi waliandika habari kwenye mitandao ya kijamii juubya kupotoshwa wa ugonjwa wa Uviko uliokuwepo Nchini hali ambayo ilipelekea kuwepo kwa taaruki kwa wananchi.
" Na sisi tunawasihi wananchi kutoamini kila habari wanayoikuta kwenye mitandao ya kijamii, na kuchukua taadhali juu ya usambazaji wa taarifa zisizokuwa na ukweli ndani yake" walisema.
Lilian Noel Ni mmoja wa watendaji wa kata waliopata mafunzo Hayo amesema kuwa wamejifunza namna ya kuwasiliana pamoja na kupata uelewa namna ya kuweza kufanya kazi na waandishi wa habari.
"Tumejifunza nyie waandishi wa habari mnatakiwa kufanya nini kwetu Kama watendaji wa kata na sisi pia tunapaswa kufanya nini kwenu Kama waandishi Hilo ndio Jambo kubwa tulilojifunza kutoka kwa internews" Alisema Liliani.
Aidha ameeleza kuwa awali hawakuwa na uelewa wowote namna ya kuwasiliana taarifa kwa waandishi wa habari na ndio maana walikuwa hawatoi ushitikiano.
"Sisi Kama viongozi wa kata hatukuwa na uelewa na namna ya kuwasiliana na kuwasiliana taarifa kwa waandishi na waandishi walikuwa hawafati Sheria taratibu na kanuni pamoja na miongozo inayowataka kupata taarifa sahihi kutoka kwa viongozi" Alisema Lilian.
0 Comments