Header Ads Widget

CHUO CHA MIPANGO NA MAENDELEO VIJIJINI CHAJA NA MWAROBAINO WA AJIRA KWA VIJANA



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma

CHUO cha Mipango na Maendeleo Vijijini kimetanua wigo wa utoaji elimu hapa nchini kwa kuanzisha kozi mpya sita ikiwemo kozi ya Tehama, uhasibu na fedha pamoja na upimaji ardhi ambapo kozi hizo  zitawasaidia vijana kujiari na kuajiwa kutokana na umhimu mkubwa wa kozi hizo katika jamii.

Mwenyekiti wa baraza la uongozi chuo cha mipango na maendeleo ya vijijini Prof ,Matha Qorra aliyasema hayo jijini hapa wakati akizungumza na wandishi wa habari katika ufunguzi wa  kongamano la kufanya mapaitio ya baadhi ya mitaala ya zaman na mitaala mipya ambayo inayoanzishwa chuoni hapo 

Alisema mitaala hiyo mipya inayoanzishwa inumhimu mkubwa katika jamii na  itawasaidia vijana kujiajiri wanyewe na kuajiriwa.

"Mitaala hiyo itakwenda kuwasaidia wanafunzi  kusoma ambapo wataweza kujiajiri na kuajiliwa kwani kozi hiyo ndizo zinatotakiwa hasa katika Kipindi hiki chansayasi na Teknolojia," Alisema Prof,Qorro.



Kwa upande wake mkuu wa chuo cha mipango na maendeleo vijijini Prof Huzen Mayaya alisema kozi zinazotolewa chuoni hapo ni bora na zinawasaidia wahitimu kujiajiri wanyewe.


"Tumekenga kuliteka soko la ajira kwa sasa kwani Kama tunavyofahamu vijana wetu wamekuwa wakisumbuliwa katika suala zima la ajira lakini kupitia kuzi hizo mpya tatizo la ajira litakuwa historian," Alisema Prof Mayaya.



Naye Makamu Mkuu wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini anayeshughulikia Taaluma,Utafiti na Ushauri Elekezi Prof Provident  Dimoso alisema kutokana na changamoto ya ajira,chuo hicho kinajikita katika ubunifu kwa vitendo ili kusaidia vijana waweze kujiajiri na kuajiriwa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI