Header Ads Widget

CHONGOLO-CHAMA CHA MAPINDUZI NI CHAMA SIKIVU KWA WANANCHI.




******************************

Katibu mkuu wa CCM Ndg.Daniel Chongolo (wa pili katikati Pichani) akimsikiliza kwa Furaha mmoja wa wanachama wa Chama cha Mapinduzi akitoa maoni yake na Furaha aliyoipata

baada ya kushuhudia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM katika moja ya wilaya za mkoa wa Kigoma Mwanzoni mwa mwaka 2022 jambo ambalo alisema Halijatokea miaka mingi na hiyo kwao kama wananchi ni kuonyesha kujali na kuwasikiliza kwa Hali ya Juu kwa Chama Hicho kwa wananchi kikiongozwa na Katibu mkuu wake.

Naye Katibu Mkuu wa CCM Ndg.Chongolo kufuatia Salamu hizo toka kwa wananchi huko Kigoma aliwasisitiza wananchi hao kuendelea kuunga mkono Chama cha Mapinduzi na Juhudi za Serikali inayoongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwani Dhamira ya CCM ni ya kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo ya kweli.

Akitaja baadhi ya Mambo ambayo CCM Imesimamia na kuhakikisha serikali inayatekeleza ni Pamoja na uendeezaji wa Miradi yote ya Kimkakati,Ujenzi wa Barabara za Lami na Changarawe maeneo Mbali Mbali ya Nchi,Upatikanaji wa Huduma za Maji Safi na salama,Upatikanaji wa Umeme,Upatikanaji wa Dawa na Vifaa tiba katika Hospitali Mbalimbali na Vituo vya Afya vya Umma Nchini,Kuimarisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao,Kuendelea kutoa Elimu Bure hadi Kidato Cha nne,Mikopo ya Elimu ya juu kwa wote wenye sifa na Mengine mengi huku akiendelea kusisitiza CCM itasimamia na kuhakikisha Ilani ya Uchaguzi 2020-2025 inatekelezwa kama ilivyopangwa huku dhamira kuu ikiwa ni kuwaletea wananchi maendeleo bila ubaguzi au kujali eneo walipo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI