Header Ads Widget

BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA LATAKIWA KUONGEZA HAMASA KWENYE MICHEZO YA WANAWAKE

 




Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Tulia Ackson @tulia.ackson amelitaka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuongeza hamasa kwenye michezo ya wanawake ili wanawake wengi zaidi washiriki kwenye michezo.


Akizungumza wakati wa kufunga tamasha la kimataifa la pili la michezo kwa wanawake jijini Dar es Salaam leo, Oktoba 22, ameviomba Vyombo vya Habari kuitangaza michezo ya wanawake ili kuwe na hamasa kubwa kama ilivyo kwenye michezo ya wanaume. 


Ameipongeza Wizara na Baraza la Michezo la Taifa kwa kutekeleza majukumu yake ya kisheria kwa vitendo ambapo amesisitiza kuwa mafanikio makubwa ya Tamasha hili ni kielelezo tosha cha juhudi zinazochukuliwa katika kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo na kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika maendeleo ya michezo hapa nchini.



 "Ndugu Wanamichezo, Niipongeze Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Baraza la Michezo la Taifa kwa kuyatekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwa kuanzisha Tamasha hili mwaka jana. Ndani ya mwaka mmoja Tamasha hili limeendelea kukua na sasa limekuwa la kimataifa kwa kushirikisha wanamichezo kutoka Tanzania bara, Zanzibar, Kenya, Uganda na Zambia". Ameongeza Mhe. Spika



Aidha, amempongeza Mheshimiwa Rais kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha na kuelekeza juu ya ushiriki wa Watanzania hususan wanawake katika michezo. 


“Mafanikio ambayo tunayaona kwa sasa katika sekta ya michezo ni matokeo ya juhudi kubwa zinazofanywa na Mheshimiwa Rais. Mathalan, sote tumeshuhudia Timu yetu ya Mpira wa Miguu ya Wanawake chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Girls), inayoshiriki kwa mara kwanza Mashindano ya Kombe la Dunia, inavyoendelea kuchanja mbuga ambapo imetinga hatua ya robo fainali.” Amefafanua Mhe. Ackson



Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Hassan Abbasi amesema dhamira ya Serikali kwa sasa ni kulifanya tamasha hilo kuwa la kimataifa kwa kushirkisha nchi kutoka mabara yote.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS