Header Ads Widget

WANAHABARI WANAWAKE WAJENGEWA UWEZO KUTAMBUA DHANA YA KIDEMOKRASIA

 


Na Amina Saidi,Matukio DaimaAPP,Tanga

Waandishi wa habari wanawake wamejengewa uwezo wa kufahamu dhana ya kidemokrasia na taasisi zinazosinamia demokrasi hapa nchini 


Mafunzo hayo yameandaliwa na chama cha wanasheria Tanganyika (TLS)kwa kushirikiana na vilabu vya waandishi Tanzania ambayo yamefanyika mjini Dodoma


Mratibu wa mafunzo hayo Selemani Pingoni amesema kuwa lengo la mfunzo hayo ni kuwajengea uwezo ili kuwawezesha kuandika habari za kweli na zenye ushahidi


"Vizuri tumehakikisha kwamba watu tunaoweza kufanya nao kazi ni waandishi wanawake kwa sababu ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari wanawake" alifafanua 

Pingoni 


Pingoni alisema kuwa inatakiwa kufahamu dhana ya demokrasia na utawala wa kidemokrasia pamoja na Taasisi zinazosimamia utawala wa kidemokrasia hapa nchini


Sambamba na madhumuni hayo ni kuhakikisha kwamba habari ambazo waandishi wanawake wanaziandika kuhusiana na utawala wa kidemokrasia ziwe ni habari zenye kiwango cha ubora kinchokubalika hapa nchini na duniani Kote


Kwa upande wake Merry Mwita ambae alikuwa mwezeshaji katika mafunzo hayo amesema kuwa wanawake hufanya kazi kwa uaminifu mkubwa 


"Nimeona mbali kwamba mkimpatia mwanamke mafunzo kwanza atatekeleza vyema na atafanya kwa uaminifu zaidi sio kwamba wanaume hawafanyi kwa uaminifu lakini wanawake wanaweza kufatilia kwa uaminifu zaidi "alisema Mwita


Pia alisema kuwa mafunzo hayo ni kwa ajili ya kuwajengea uwezo ili waweze kuripoti vizuri kuhusu masuala ya sheria,Sera na kuweza kugusa mihimili muhimu kama vile Makama naBunge chini ya uchaguzi lengo ni kuwapatia wananchi habari zilizo sahihi


Nae Monica Msomba ni miongoni mwa waliohudhuria mafunzo hayo amesema kuwa mafunzo hayo yamemjengea uwezo wa kuandika habari za sera,kanuni na sheria 


"Kitu ambacho kimenivutia ni pale ambapo mwezeshaji ametukumbusha ni wajibu wetu waandishi wa habari tunapokuwa tunaandika storitunarejea kwenye sheria sera na katiba ili kuipa stori yako nguvu"alisema Msomba 


Msomba amesema kuwa ameweza kujifunza na kujua taasisi za kidemokrasi pamoja na masuala ya utawala wa kidemokrasia ambapo mwanzo alikuwa akiona ni vitu vigumu katika kuandika stori zinazohusu sheria.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI