Header Ads Widget

UWT KIBAHA MJINI WAPATA VIONGOZI WAPYA.

 


JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake Tanzania ya Chama Cha Mapinduzi CCM (UWT) Wilaya ya Kibaha Mjini imemchagua Eline Mgonja kuongoza Jumuiya hayo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.


Mgonja amefanikiwa kutetea kiti chake baada ya kupata ushindi wa kishindo wa kura 165 kati ya kura 237 zilizopigwa kwenye uchaguzi wa Jumuiya hiyo.


Uchaguzi huo ambao ulifanyika Picha ya Ndege Wilayani Kibaha Mgonja aliwabwaga washindani wake wawili Batuli Maelo aliyepata kura 72 na Caroline Malekela akipata kura moja.


Msimamizi wa uchaguzi huo Nasir Mkalipa alisema kuwa idadi ya wapiga kura ilikuwa 238 ambapo kura moja iliharibika  na kufanya kura halali kuwa 237.


Mgonja alisema kuwa lengo lake kuu ni kumkomboa mwanamke ili kumwondoa asiwe  tegemezi kuwa na ushirikiano pamoja na kuachana na dhana kuwa mwanamke hawezi lakini wanaweza wanapaswa wajiamini na wasikate tamaa kuna kuchafuliwa na kusemwa vibaya wakati wa uchaguzi lakini wanapaswa kupambana ili kufikia malengo yao.


Naye Katibu wa UWT Kibaha Mjini Mariamu Mugasha alisema kuwa mara baada ya uchaguzi wanatarajia uongozi mpya kukamilisha jengo la kitega uchumi ambalo limefikia kwenye linta ili likamilike.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI