Header Ads Widget

THERESIA KOMBA MWENYEKITI MPYA UWT MANISPAA YA MOSHI.

 


NA WILLIUM PAUL, MOSHI.


WANACHAMA wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamemchagua Theresia Komba kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo.



Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni Katibu wa CCM wilaya ya Moshi mjini, Ibrahimu Mjanakheri alisema kuwa kura zilizopigwa na 175.



Mjanakheri alisema kuwa, Salma Kabwe alipata kura 19, Ummy Ndoile alipata kura 34 na Theresia Komba aliibuka mshindi kwa kupata kura 122.


Katika uchaguzi huo aliyekuwa Mwenyekiti, Lugreshi Kundi alichaguluwa kuwa Mjumbe wa mkutano mkuu wa UWT Taifa.



Akitoa shukrani kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti, Theresia aliahidi kuendeleza ushirikiano uliopo katika Jumuiya hiyo.



Alisema kuwa, katika kipindi chake cha uongozi cha miaka mitano ndani ya Jumuiya hiyo atashirikiana na wanachama wa Jumuiya hiyo pamoja na wanaccm kuhakikisha malengo ya Jumuiya pamoja na chama yanafikiwa.



Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Kilimanjaro, Zuhura Chikira alipongeza jinsi ambavyo uchaguzi huo ulivyoendeshwa kwa huru na haki na kuwapongeza wale wote waliochaguliwa.



Alisema kuwa jukumu la kila mwananchi wa Umoja huo kwa sasa ni kutoa ushirikiano kwa viongozi waliochaguliwa kwani kufanya hivo kutapelekea kazi yao kuwa nyepesi ya kuongoza Jumuiya.

Mwisho...

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI