NA TITUS MWOMBEKI , Matukio Daima App Kagera.
SHIRIKISHO la Vyama Vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Kagera imewaomba watu wenye ulemavu pamoja na wazazi wenye watoto wenye ulemavu kujenga utamaduni wa kutembelea ofisi za shirikisho hilo zilizopo katika Manispaa ya Bukoba mkabara na ofisi ya Takwimu mkoa ili kuwasilisha changamoto zao kwa viongozi wao.
Hayo yamesemwa katibu wa shirikisho hilo, Sweetbert Mushanga wakati akiongea na chombo hili ofisini kwake ambapo amesema kuwa muamko wa watu wenye ulemavu kutembea ofisi za shirikisho hilo bado ni mdogo huku akiwataka watembelee ofisi hizo ili kuwasaidia viongozi wao kubaini changamoto zinazowakumba nao waweze kuziwasilisha kwa wafadhiri wao pamoja na serikali.
“Bado muhamko wa watu wenye ulemavu pamoja na wazazi wenye watoto wenye ulemavu kutembelea ofisi zetu ni mdogo, lakini wanatakiwa kuwa wanatembelea ofisi zetu ili tuweze kutambua changamoto zao nakuziweka katika rekodi zetu ili tunapopata wafadhiri tujue tuna uhitaji wa vifaa gani, vingapi na kwa watu wangapi wenye uhitaji”
“Unaweza kukuta hata halmashauri zetu zinatamani sana kutusaidia ila sasa zinashindwa kufanikisha kutokana nakushindwa kujua wapi pa kutukuta kwa pamoja nakusikiliza changamoto wetu kwa pamoja”
Ameongeza kuwa, mpaka sasa CHIVYAWATA wamepokea maombi ya watu nne ambao wanahiji vifaa saidizi zikiwepo baiskeli, fimbo nyeupe, kofia pamoja na mafuta ila bado vifaa hivyo havijapatikana.
Kwa upande Albert Christian wa amesema kuwa, kutembelea ofisi za shirikisho hilo na kuwasilisha kero zao ni wazo zuri kwani wafadhiri wanapokuja wanaangalia kama wahitaji ni wengi ndipo wanapoamua kusaidia.
Naye Geofrey Method mkazi wa mtaa wa Omukishenyi kata ya Hamugembe Manispaa ya Bukoba amewashauri viongozi wa shirikisho hilo kuwa wanatakiwa kuongeza mabango kando kando ya barabara ili kurahisisha watukujua ofisi zao zilipo.
0 Comments