NA HADIJA OMARY LINDI
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack amemtaka Ofisa Elimu wa Mkoa huo Richard Kayombo kuandaa mkakati maalum wa Elimu ya watu wazima ili Mkoa huo uendelee kufanya vizuri katika Sekta hiyo ya Elimu kama unavyofanya kwenye Elimu rasmi.
Akizungumza katika kilele cha juma la Elimu ya watu wazima kilichofanyika Halmashauri ya mtama Mkoani Lindi, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo alisema ili maadhimisho hayo yaweze kuwa na tija ni wajibu wa kila mdau kutambua na kuthamini mchango wa Elimu ya Watu wazima kwa maendeleo ya TaifaAlisema Mkoa wa Lindi umekuwa ukishika nafasi za juu katika matokeo yake ya mitihani mbali mbali hali inayowafanya baadhi ya watu kuja kujifunza mambo kadhaa kutoka kwao ya namna Mkoa huo unavyofanikiwa.
“ Ofisa Elimu upo hapa wewe ni mahiri sana umeukomboa Mkoa huu mpaka sasa katika maeneo mengi tumekuwa wa kwanza , kidato cha sita mkoa wa kwanza, kidato cha nne mkoa ni wa kwanza , kidato cha pili tunakuwa watatu mpaka wa pili, kidato cha nne tunakuwa kwenye nafasi mziri ”
“Tumepunguza daraja sifuri , tumeongeza daraja la kwanza , lapilli na latatu tumepunguza sana daraja la nne na juzi tulikuwa kwenye mkakati wa kuhakikisha tunafuta kabisa daraja sifuri , sasa kwa nguvu hiyo hiyo tukuone sasa unaandaa mkakati maalum wa Elimu ya watu wazima katika Mkoa wa Lindi” alisema Ndemanga
Ndemanga alisema licha ya Serikali kuweka program kadhaa katika Elimu ya watu wazima zinazolenga kukabiliana na changamoto za maisha lakini katika Mkoa wa Lindi shughuli za utoaji wa Elimu ya watu wazima bado hazijashika kasi ya kutoshaHalmashauri kupitia maofisa Elimu ya watu wazima hawaonyeshi harakati za kuhakikisha , kuanzisha, kusimamia, pamoja na kutekeleza ufuatiliaji wa program za elimu ya watu wazima .
Alisema ni wajibu sasa kwa maafisa Elimu ya watu wazima wa halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha Elimu hiyo ya watu wazima inakuwa hai kwa kuanzisha, kusimamia sambamba na kufuatilia utekelezaji wa program za elumu za watu wazima.
Kwa upande wake Ofisa Elimu Mkoa wa Lindi, Richard Kayombo Alisema Mkoa huo una jumla ya taasisi 14 zinazojishuhulisha na utoaji wa Elimu ya watu wazima nje ya mfumo usio rasm zilizopo katika maeneo mbali mbali ya halmashauri za Mkoa huo .
Hata hivyo Kayombo alitumia fulsa hiyo kuwahasa watu wazima na wanajamii hususani vijana na wanafunzi kutumia fursa zilizopo katika Mkoa huo kujifunza na kujiendeleza katika taasisi mbali mbali za serikali na sisizo za kiserikali ndani ya ili kujikwamua na adui ujinga.
Naye Mkufuzi mkazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wazima Mkoa wa Lindi, Hassan Mgomba alisema kuwa pamoja na mambo mengine kwa sasa taasisi hiyo inatekeleza program ya kuwasaidia wasichana waliokatisha masomo ya sekondari kutokana na changamoto mbali mbali kuanzia miaka 13 mpaka 21.
Alisema katika program hiyo Serikali inawasaidia wanafunzi waliokuwa tayari kurudi shuleni kwa ajili ya kuendelea na masomo kuwalipia ada pamoja na vifaa mbali mbali vya shule.
0 Comments