Header Ads Widget

POLISI IRINGA WAUA WATUHUMIWA WA UJAMBAZI WATANO ....

 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi akionesha silaha walizotumia watuhumiwa wa ujambazi watano kabla ya kuuwawa na wengine 7 kutoroka ,kushoto ni mkuu wa wilaya ya Mufindi Saad Mtambule.

:::;;:;;;;;;;;;;::::;;;;;;;;;;;;;;:::::::::::::;;::::;;;;;:;;;;;;;;;;

WATUHUMIWA  watano kati ya 12 wa tukio la ujambazi wameuwawa na jeshi la Polisi mkoani Iringa wakati wa majibizano ya risasi baada ya watuhumiwa hao kuvamia kiwanda Cha Daashong kilichopo Kata ya Changarawe Wilayani Mufindi .Na Matukio DaimaAPP Mufindi 


Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Iringa Allan Bukumbi aliwaeleza waandishi wa habari leo   kuwa tukio hilo limetokea  Saa 8  usiku wa kuamkia Septemba 30  mwaka 

Kamanda Bukumbi alisema jeshi la Polisi lilipata taarifa kutoka Kwa raia wema kuwa Kuna watuhumiwa wa ujambazi wanapanga njama ya kwenda kuvamia kiwanda hicho usiku na Polisi waliweka mtego uliowanasa wahusika hao .

Kuwa majira ya Saa 2 usiku watuhumiwa hao wa ujambazi wapatao 12 walifika eneo la tukio wakiwa tayari kuvamia kiwanda hicho na Polisi waliwataka wahalifu hao kujisalimisha lakini walikaidi Amri na kuanza kuwarushia risasi askari.

Kamanda Bukumbi amesema baada ya majibizano hayo ya risasi wahalifu watano walijeruhiwa na wengine 7 walifanikiwa kutoroka .

Amesema Katika tukio hilo silaha mbili zimepatikana moja ikiwa ni shotgun na nyingine ikiwa ni Pump Action pia yalipatikana mabegi mawili ya magodoro  begi moja ndani kulikuwa na sare za jeshi la wananchi Tanzania na risasi za shotgun 13.


Wakati begi la pili lilikuwa na sare za JKT ,Jaketi moja la mtumba linalofanana na kombati ya jeshi ,shoka moja ,na kitambaa kimoja kinachofanana na kombati ya jeshi ,pia zilikutwa line za simu za mitandaa mbali mbali  Tigo zikiwa 12 na Airtel 25 na voda 7 .

Kamanda Bukumbi amesema Majeruhi hao walifariki Dunia wakati wakikombizwa Hospitali ya mji wa Mafinga Kwa matibabu zaidi kutokana na majeraha ya risasi waliyoyapata .

Aidha kamanda Bukumbi ameonya wale wote wanaojihusisha na Matukio ya uhalifu Kwa Kupanga kuja Iringa kuwa hawatafanikiwa kufanya uhalifu huo .


Wakati huo jeshi la Polisi mkoa wa Iringa linawashukuru wananchi wote wanaoendelea kutoa ushirikiano Kwa jeshi Hilo Kwa kufichua uhalifu na wahalifu na kuwataka wote wanaomiliki silaha kienyeji kusalimisha silaha zao vituo vya Polisi.

Mkuu wa wilaya ya Mufindi Saad Mtambule ambae ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Mufindi alipongeza jeshi la Polisi Kwa kazi nzuri na kuwa Kwa wiki nzima hii kumekuwepo na Matukio mfulilizo ya uvamizi wa kutumia silaha.


Hivyo kuuwawa Kwa washukiwa hao watano ni hatua kubwa ya kupambana na uhalifu ndani ya Wilaya ya Mufindi .

Mtambule alisema kuanzia Sasa tayari wenyeviti wa Serikali za vijiji na mitaa wameelekezwa kuanza misako ya kuwafichua wageni wote ambao hawatambuliki.










Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI