Header Ads Widget

KUNA HAJA YA KUBADILI SHERIA KWA MTU ALIYETAKA KUJIUA-DR TAWALA


 Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma

MKURUGENZI  wa Hospital ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe Dkt Paul Tawala amesema kuna haja ya kubadilishwa kwa Sheria ya makosa kwa mtu aliyetaka kujiua badala ya kuchukuliwa kama ni mkosaji au mvunjaji wa Sheria achukuliwe na kutibiwa afya yake na sio kumuona mhalifu.


Amesema hayo Jijini hapa wakati akizungumzia na waandishi wa habari katika siku ya matembezi ya hisani ya kuhamasisha Afya ya akili ambapo alisema kila ifikapo tarehe 10 Septemba ni siku ya kuzuia kujiua duniani.


Ameeleza wao Kama hospital ya Taifa ya Afya ya akili wameona kuna haja ya kukaa pamoja na watunga Sheria,Sera  bungeni ambao ndio wabunge kuzungumzia Sheria na adhabu anayotakiwa kupatiwa mtu aliyetaka kujiua kwani takwimu kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) zinasema ndani ya sekunde 40 kuna mtu anafikilia kujiua.

 

"Tunatakiwa tutazame zaidi nini kitu kilichomfanya mtu huyo ajinyonge sasa kuliko kwenda kumbana na kuchukuliwa mtu huyo ni kama mhalifu akapimwe Afya yake," alisema Mkurugenzi huyo.


Anaelezpa dhana ya kujiua inavyohusiana na afya ya akili .


Amesema dhana ya kujihisia Afya ya akili ni dhana ya fikra na hisia ambapo kunakuwa na mabadiliko ya tabia Mtu ambaye anakuwa na mpango wa kujiua anakuwa na mambo ambayo yalimtangulia na kumshinda na Kadri ubongo unavyofanya kazi ndivyo anakuwa kwenye hatari ya kujiua zaidi.


"Wengi wanakuwa na hisia hasi kutokana na Matukio yaliompata wakati ule mtu anakuwa na jambo kubwa ambalo anashindwa kukabiliana nalo na kuona maisha hayana thamani taifa na familia limemuacha kakataliwa na kila mtu Hali inayopelekea kukata tamaa na anapofika mwisho ndio inapelekea kujua,"amesema


Hata hivyo alilisisitiza suala zima la elimu itolewe katika jamii ili kuweza kuzuia vitendo vya kujiua .


Naye mgeni Rasmi katika katika Matembezi hayo Mbunge wa Iringa Mjini Jesca Msavatavangu amesema tatizo la Afya ya akili ni tatizo kubwa na wanaoathilika zaidi ni vijana kuanzia umri wa Miaka18 hadi 25.


"Kundi hilo ni kundi la vijana na ndio nguvu Kazi ya Taifa hivyo sisi Kama jamii tukiaa kimya bila Kuongea na kuzungumza na watoto wetu juu ya matatizo ya Afya ya akili ndipo wanapokwenda kukutana na makundi maovu na kuwahusisha kwenye Kazi zisizofaa na kupelekea Kuwa na vijana katili na wenye maamuzi ya hivyo," amesema Mbunge huyo.


Kwa Upande wake Mkaguzi kutoka Jeshi la Polisi Veridiana Mlimba amesema nia ovyu inaanza ndio kinafuata tendo ovu hivyo kuna  umuhimu wa kupata elimu ya Afya ya akili.


Amesema Jeshi la Polisi linashukuru kwa kualikwa katika tukio hilo kwani akili za Watu katika jamii zikiwa sawa uhalifu na vitendo vya kikatili vinapungua .


"Sasa hivi tunashudia watoto wanaoanza kukua kuanzia 14 hadi 22 ndio wanatatizo kubwa kwani wengi wanajiingiza kwenye makundi na Magenge ya kihalifu na wamekuwa wakiingia kwenye makundi hayo ya hovyo kutokana na kukosa watu wa kukaa nao na kuwashauri juu ya Afya ya akili ili kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi kulingana na Mazingira yao 


Na kuongeza"Tukisimama pamoja Kama jamii na wadau hata haya makundi ya Panya Road, Panya Kaloa yatapungua katika taifa letu,"amesema Mkaguzi huyo.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI