Header Ads Widget

HakiElimu YAZINDUA RIPOTI YA UTAFITI , YABAINI CHANGAMOTO, YATOA MAPENDEKEZO

 

Na  Matukio Daima APP Dar es Salaam

Asasi ya HakiElimu leo imezindua matokeo ya utafiti katika ngazi ya elimu ya uraia Shule za Sekondari na Ushiriki wa Vijana katika Demokrasia nchini  ambapo umeonesha elimu ya uraia inayotolewa  shuleni ina mchango  kidogo katika kumsaidia kijana wa kitanzania kujifunza na kushiriki shughuli za kisiasa na demokrasia. 


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akizindua ripoti ya utafiti huo, Kamishna wa Elimu  Dk Lyabwene  Mtahabwa amesema kuwa utafiti huo umekuja wakati muafaka ambapo Rais Samia ametoa maagizo yafanywe mapitio ya mitaala ya elimu ya Tanzania Ili kuwajengea uwezo wanafunzi waweze kuona fursa katika mazingira yao na waweze kujitegemea.



Aidha, katika kujenga demokrasia ya kweli ni lazima ipewe uzito wa hali ya juu kwa kumpa mtoto thamani yake ya utoto na kumuacha afurahie utoto wake , huku akiitaka jamii kuonesha uzalendo wa kweli ule ambao unatoka moyoni Ili kwa pamoja tuweze kuimarisha ulizi na usalama wa mtoto popote atakapokuepo afurahie utoto wake.


"Nimeyaona mapendekezo yaliyopo katika utafiti niliouzindua leo ni mazuri mno na yamekuja kwa wakati muafaka tutayabeba na kuyazingatia nitayapeleka katika kamati ya kitaifa iliyoundwa kupitia mitaala ya masomo na sasa tupo katika hatua nzuri "amesema Dk Lyabwene.


Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi HakiElimu Godfrey Bonveture amesema kuwa,utafiti uliofanyika na Asasi ya HakiElimu umebaini kuwepo kwa changamoto kubwa katika mtaala wa somo la uraia Shule za Sekondari ambao kwa kiwango kikubwa haumpi  mafunzo stahiki Mwanafunzi yatakayomfanya aelewe vyema namna ya kushiriki shughuli za kidemokrasia.


Aidha, amesema, kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa kwa wilaya 10 umeonesha ushiriki hafifu kwa vijana katika mifumo ya kidemokrasia ndani na nje ya shule ambapo asilimia 44.4 wanafunzi hawaelewi maana ya demokrasia huku asilimia 85.5 hawajawahi kushiriki wala kushirikishwa katika vikao rasmi vya maamuzi kuhusu mapato na mgawanyo wa rasilimali za shule .


"utafiti huu pia umeonesha asilimia 47 ya viongozi wa wanafunzi shule za Sekondari hawapatikani kwa njia ya chaguzi za demokrasia bali kwa kuteuliwa na uongozi wa shule,huku katika ngazi ya jamii zaidi ya asilimia 80 ya vijana walioko shuleni hawajawahi na hawahamasishwi kushiriki mikutano ya kampeni na siasa"amesema Bonveture. 


Aidha, wazazi na walezi wametakiwa kuachana na mfumo wa malezi usiowashirikisha watoto au unaowatenga katika maamuzi ya kifamilia na maslahi yao, pamoja na kuwashirikisha watoto katika kuchagua katika masuala mbalimbali ikiwemo elimu, fani, upangaji wa bajeti za kifamilia na uendeshaji wa mipango ya kifamilia kidemokrasia badala ya kuamuliwa kila kitu.


Hata hivyo, wameiomba Serikali kuboresha ufundishaji wa somo la uraia darasani kwa kusisitiza Mawasiliano ya karibu zaidi kati ya Mwalimu na Mwanafunzi na kuchanganya mbinu za darasani na nyengine kama matumizi ya magazeti vipindi vya radio na Tv na kuwashirikisha watoto katika vikao au shughuli zinazohusisha siasa za demokrasia katika ngazi ya shule.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI