Na Gabriel Kilamlya,Matukio DaimaAPP NJOMBE
Wakati shughuli ya Sensa ya watu na makazi ikitarajia kukamilishwa hapo Septemba 1 mwaka huu,Mkoa wa Njombe unatarajia kuhesabu jumla ya majengo 296625 pamoja na barabara 5179.
Mkufunzi mkuu na Msimamizi mkuu wa sensa ya watu na makazi mkoa wa Njombe bwana Saruni Njipay amesema kukusanywa kwa taarifa za makazi hayo na barabara kutalisaidia taifa katika kupanga mipango ya maendeleo ili kuwasaidia wananchi wake.
Mratibu wa sensa ya watu na makazi mkoa wa Njombe bwana Israel Mwakapalala amesema sensa ya makazi inahusisha majengo yote yaliyokamilika na ambayo hayajakamilika kwa maana ya maboma hivyo wamiliki wanapaswa kuandaa taarifa za majengo yao au kuwaachia wapangaji wao.
Kituo hiki kimewatembelea baadhi ya wananchi waliofikiwa na zoezi hilo akiwemo Marry Sanga ambao wanasema wanaamini serikali ina lengo nzuri na wananchi wake kwani hata maswali wanayoulizwa na makarani hayana ukakasi wowote.
Changamoto kubwa katika kazi ya sensa ya makazi imetajwa na baadhi ya makarani akiwemo Makway Barani kuwa ni baadhi ya wamiliki wa nyumba kutoacha taarifa za nyumba zao kwa mtu yeyote pindi wanapokuwa hawapo.
Septemba mosi mwaka huu zoezi la Sensa ya watu na makazi linafikia tamati kwa kuhesabu majengo baada ya sensa ya watu kufanyika siku chache zilizopita.
0 Comments