NA HADIJA OMARY, MATUKIODAIMAAPP
LINDI
MKUU wa Wilaya ya Lindi, shaibu Ndemanga amewataka wadau wanaohusika na zoezi la utoaji wa chanjo ya polio kwa Watoto walio chini ya umri wa miaka 5 inayotarajiwa kuanza kesho September 1 hadi 4 2022 kuhakikisha wanayafikia maeneo yote magumu ambayo yameainishwa na kutambuliwa na Wilaya hiyo ikiwemo maeneo ya wafugaji.
Ndemanga ametoa agizo hilo leo Agost 31 2022 alipokuwa anafungua kikao cha afya ya msingi ya jamii juu ya kampeni ya kitaifa chanjo ya polio awamu ya tatu kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya kamishina wa Aridhi Manispaa ya Lindi Mkoani humo
Ndemanga alisema Ili kufikia lengo la utoaji wa chanjo ya polio kuwafikia watoto wote wenye umri chini ya miaka 5 katika Wilaya hiyo , Serikali Wilayani humo imeweka mpango Madhubuti ikiwa pamoja na kubainisha na kuyatambua maeneo ambayo ni magumu kufikika lengo likiwa ni kufikia Watoto wote waliopo katika Wilaya
alisema kuwa katika kampeni hiyo licha ya kuwafikia Watoto wa maeneo mengine wanakwenda kuweka mkazo kwa wafugaji ambao wanahama hama pmoja na kuingia wapya katika maeneo hayo.
“Tumebaini kwamba kuna Watoto wengi sana walio chini ya miaka mitano katika maeneo ya wafugaji ambao kwa hali yoyote ni lazima wapate chanjo na kwa sababu wanahama hama wakipata tatizo ni rahisi kulisambazo katika maeneo mengine”alisema Ndemanga.
Aidha Ndemanga pia lisema kuwa miongoni mwa makundi ambayo yanawapa shida kuyafikia katika maswala mbali mbali ni kundi hilo la wafugaji na kwamba
Kwa upande wake kaimu mganga Mkuu wa Manispaa ya Lindi, Abilah Mbingu alisema kuwa katika kampeni hiyo ya Chanjo ya polio manispaa hiyo inatarajia kutoa chanjo kwa Watoto 36,098 waliochini ya umri wa miaka 5
Mbingu alitumia fursa hiyo kuwahasa wazazi na walezi kuwatoa Watoto wao katika zoezi hilo ili Waweze kupata chanjo kwani chanjo hiyo ni salama na haina madhara kwa Watoto
Kwa kupande wake mratibu msaidizi wa chanjo Manispaa ya Lindi, Mahuto Masalu alisema kuwa katika utekelezaji wa kampeni hiyo tayari wameshapokea jumla ya dozi 40,000 za polio pamoja na vifaa vingine muhimu na kusambazwa katika vituo vyote vya kutolea huduma.
Hata hiyo alisema kuwa katika maeneo ambayo yanaugumu kufikika uwa wanatumia mbinu mbali mbali kuyafikia kama vile piki piki ama mtoa huduma kuweka kambi katika Eneo husika.
Amina ally ni Mkazi wa manispaa ya Lindi ameahidi kutoa ushirikiano kwa kumpeleka mtoto wake hapo kesho ili kupata chanjo hiyo huku akiwasihi wazazi na walezi kupuuza taarifa za upotoshaji wa baadhi ya wananchi juu ya chanjo zinazotolewa na Serikali
0 Comments