Header Ads Widget

WAUWAWA KISHA MIILI YACHOMWA MOTO WAKITUHUMIEA WIZI WA NG'OMBE

 


Na Mapuli Misalaba,Matukio DaimaAPP Shinyanga

Watu wawili  wameuawa kwa kupigwa na kisha miili yao kuchomwa moto na watu wenye hasira kali , baada ya kutuhimiwa kwa wizi wa Ng’ombe katika kijiji cha Mwamala (B) kilichopo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.


Mtendaji wa Kata ya Mwamala Suzana Kanyange amesema kuwa, tukio hilo limetokea majira ya saa 12:30 asubuhi ya leo, ambapo watu hao walizingirwa na wananchi baada ya kutuhumiwa kuwa wamekuwa wakijihusisha na matukio ya wizi wa Ng’ombe kijijini hapo.


 Amewataja waliouawa kuwa ni, Simbili Philipo Izengo mwenye umri wa miaka  33 na Kashinje Malulu mwenye umri wa miaka 32, ambao wote ni wakazi wa kijiji cha Mwamala (B) katika halmashauri hiyo ya wilaya ya Shinyanga

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI