Na Zulfa Alfan, Matukio DaimaAPP Simiyu
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Lupakisyo Kapange amewataka wanamichezo kujitokeza kushiriki Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika August 23 mwaka huu.
Kapange ameyasema hayo leo wakati akifunga Bonanza la Michezo lilioandaliwa na Kituo Cha Radio Bariadi FM kilichopo mjini Bariadi.
Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, (Dkt. Yahaya Nawanda), Kapange amesema lengo la Serikali kufanya Sensa ya Watu na Makazi ni kutaja kujua idadi yao Kwa lengo la kuwaletea maendeleo.
"Nawasiistiza tushiriki kikamilifu zoezi la Sensa ya Watu na Makazi, Kila Mwana Simiyu awe tayari kuhesabiwa..." Amesema Kapange.
Katika hatua nyingine Kapange amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo kuhakikisha wanarekebisha viwanja vya michezo li viweze kutumika Kwa michezo mbalimbali na wataweza kuibua vipaji vya vijana.
Amesema serikali inatambua jitihada zinazofanywa na wadau wa michezo mkoani humo huku akiwaagiza maafisa michezo kutoa elimu juu ya masuala ya michezo ili kuukuza mkoa huo kimichezo.
Awali Mkurugenzi wa Bariadi FM, Samada Maduhu amesema mashindano hayo yamejumuisha timu 32 za Mkoa wa Simiyu wakati kauli mbiu ya mashindano hayo ni Usalama Kwa Maendeleo.
Katika Mashindano hayo timu ya Red Buffalo imekuwa bingwa wa Mashindano hayo Kwa kuifunga timu ya Black Scopion goli 3-1.
Timu ya Red Buffalo imechukua kombe na shilingi milioni 1.5, huku timu ya pili ya Black Scopion ikipata Shilingi 600,000/=, Ikungulyandili 350,000/= na Ntenga Fc ikipata 200,000/=
0 Comments