Na Esther Machangu , MatukioDaimaAPP,
Moshi
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, Adolph Mkenda, ametoa Onyo kwa shule za binafsi ambazo Bado hazijawaruhu wanafunzi kurudi nyumbani Ili Kushiriki zoezi la Sensa Ambalo linatarajiwa kufanyika Agosti 23,
Akizungumza na waandishi wa Habari Mkoani hapa Agosti 21, amesema anatoa Onto Kali kwa baadhi ya shule Binafsi ambazo hazifuati Maagizo ya Serikali
"Tumepata taarifa kuwa baadhi ya Shule binafsi Bado hazijafungwa,sasa shule nyingi za Kanda hii zimefungwa ila tumepata taarifa kuwa Bado Kuna baadhi ya shule binafsi hazijafungwa"amesema
Amesema Baadhi ya shule Binafsi wamepanga kufunga shule Agosti 22 Ili Agost 23 wakaesabiwe, na kuongeza kuwa Serikali inapenda kushirikiana na Sekta binafsi kikamilifu, ila hawana budi kufuata matakwa ya Serikali.
"Chukulia mfano mtoto anatoka mikoa ya Mbali kama ruvuma au kagera alafu mnafunga shule tarehe 22, je ni lini atafika nyumbani Ili Kushiriki zoezi la Sensa, alafu arudi tena shule tarehe 24, huku ni kumchosha mwanafunzi, Serikali isingependa kutoa kauli za kufukuzana,kuwindana na kutoa Maelekezo mazito sana"amesema
Wito wangu kwa Hizi baadhi ya Shule Binafsi wanafunzi wote wawe Majumbani na Raisi Samia Suluhu amesema kuwa siku ya Agosti 23 ni Mapumziko, hivyo ni vyema Kuheshim Hilo.
"Kwa watakao kiuka agizo hilo Kuna Sheria ambazo tutazitumia kwa wakuu wa Shule na Wenye shule ambao hawafuati agizo Hilo"amesema
Mwisho.....
0 Comments